Ushauri tafadhali, mke wa mtu ananisumbua sana

davetz 23

JF-Expert Member
Oct 10, 2016
206
302
Naombeni ushauri, mimi ni mume wa mtu pia ni mtumishi na mwenye maisha ya kawaida sana yaani dola mbili kwa siku ndio maisha yangu na ninashukuru ninaridhika ninachopata.

Niinapofanya kazi kuna wanawake wengi sana kwa idadi tofauti na idadi ya wanaume ambayo ni karibia theluthi moja ya watumishi wote hapa.

Shida yangu ni kwamba kuna mmama age 40+ mke wa mtu ananisumbua sana, alianza muda sana karibu miaka miwili iliyopita aliniambia wazi kuwa ananipenda ila sikumjibu chochote na kila tukikutana stori zake ni hizo hizo na mimi sina mpango naye japo ni mrembo.

Sasa shida ni kwamba sasa hivi hataki stori kabisa na mimi hata mambo ya kazini kama kuna jambo linalohusu kazi ukimwuliza hataki kusema na mimi.

Kwa ujumla sitaki kuishi kwa uhasama na mimi pia sihitaji kuingiza mapenzi kwake kwa sababu najua athari ya mapenzi kazini.

Naomba ushauri nifanyeje kwa mama huyu?
 
Achana nae usikubali kuingia huo mlango ndani utakuta matatizo tu, she is wicked, na ukimruhusu ataiwinda ndoa yako ili aiangushe
 
Back
Top Bottom