Ushauri tafadhali, aliniambia ana ujauzito wangu nilimkataa

Madihani

JF-Expert Member
Apr 30, 2015
6,083
6,921
Habari JF,

Mwaka 2014 nilikuwa na uhusiano ni binti kwa muda mfupi kama wiki mbili hivi.Kuna siku alinipigia simu akaniambia hajapata hedhi na ameamua kupima majibu yanaonyesha ni mjamzito.

Mimi nilikataa nikamwambia unataka kunipakazia mzigo.Alilaumu na kukubaliana na majibu yangu.

Sasa marafiki zangu wananiambia yule binti kuwa alijifungua mwaka jana 2015 na mtoto anafanana na mimi.Yani ni mtoto wangu.

Ushauri nifanyeje ili niweze kuanza taratibu za malezi ya mtoto.
 
Kutokana na hali ilivyo huyo binti atakua na hasira sana na wewe, ukijipeleka mwenyewe watakuona mhuni tu. Tafuta mtu aliekuzidi umri unaemuona anabusara mfano baba yako, mjomba, kaka aende akakusaidie kuomba msamaha kwa binti ikiwezekana na familia yake. Binti na familia wanaweza kukuuliza una mpango gani na mama na mtoto? Ujiandae kujibu hilo swali.
Kama ulivyosema awali mlifahamiana katika kipindi cha wiki mbili, ni wazi nyinyi wawili hamfahamiani vizuri lakini kuna kiumbe kinawaunganisha. Umeshaoa?
 
Kwa hakika wanadamu ni watu wanafiki sana....unaweza kukuta mtoa mada ni miongoni mwa watu wanaolalamikia ongezeko la watoto wa mitaani au wale wanaoishi katika mazingira magumu........
Sisi wanaume tuna kila sababu ya kutupiwa lawama kwa namna moja au nyingine katika hili seke seke la watoto wa mitaani.......kwani ni wanaume wengi sana wanazikataa mimba kwa visingizio visivyo na kichwa wala miguu.......baadhi ya wanawake shupavu wanajikuta wanapambana na majukumu ya malezi peke yao huku wewe ukiponda raha......

Wanamume tubadilike
 
yawezekana ulivyoikataa wewe kuna mtu alibambikiwa na akakubali kuilea na kugharamia so kabla hujaanza lolote fanya utafiti wa hilo kwanza ukigundua kuna mwanaume alilea piga kimya tu mpaka baadae huko
 
We naona unataka kuwa ka baba diamond , baba kazi yake kumenya viaz mwanae msanii mkubwa africa , ni hv mwanamke akikwambia mimba yako na anataka kutoa kataa kama ni kuzaa kubal ni ngumu kusingiziwa mtoto
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom