Ushauri - suzuki swift

BABA E's

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
354
Reaction score
137
Habari wataalam,

Nimekuwa na suzuki swift kwa karibu miaka miwili sasa, lakini siku za hivi karibuni imeanza kunifanyia mchezo ambao hata mafundi wanashindwa kuuelewa. Tatizo ni kuzimikazimika, yani inakera mpaka basi, unapotembea kila baada ya dakika kama 20 inazimika na inawaka kwa tabu sana, kama vile mafuta hayafiki. Baada ya muda inakubali ukiendelea tena dakika kama hizo tatizo linajirudia. Tumeshajaribu kubadilisha fuel pumb, relay na vituvitu vingine, lakini tatizo lipo pale pale, kifupi nimeshaingia gharama sana lakini tatizo bado lipo. Sasa sasahivi mafundi wananiambia kwamba kuna sensor za kubadilisha, na wanasema craneshaft sensor ndio itakuwa tatizo.

Sasa wandungu naomba ushauri kama kuna mtu ameshawahi kupata hilo tatizo, maana sasahivi ni kama tunabahatishabahatisha na hawa mafundi wangu wa mitaani.
 
Mdau umenitisha maana nilikuwa nikalipie swift kwenye mtandao. Kama hutajali vip spares ni bei kulinganisha na Toyota?
 
mkuu nozel umecheki au umezisafisha kama si kubadilisha...
 
IInawezekana kabisa ikawa ni sensor.swift inq sensor mbili kweye engine kwa juu kidogo ambazo ikiingia maji ndio shida inaanzia hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…