Ushauri, Serikali isivunje mikataba ya madini isipokuwa i-regenotiate

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,896
1,862
Habari za Ijumaa Ndugu,

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa matukio yanayoendelea hapa nchini hususani hili la Madini, mikataba na sintofahamu iliyopo na inayoendelea kuwepo, binafsi nina maoni tofauti kidogo na baadhi ya watu na nitaeleza nini maoni yangu katika hili.

Binafsi nimeshtushwa sana na trend inayoanza kupata chat kuwa kila anayetoa mtazamo tofauti na ule uliochukuliwa na Mh Rais anaonekana kama kibaraka fulani hivi, asiyeitakia mema nchi, kibaraka wa wazungu na mengineyo mengi. Imani yangu ni kuwa wanaojaribu kutoa hoja tahadharishi si tu kwamba wanaitakia mema nchi bali wanatimiza jukumu muhimu la kuishauri serikali ambayo makosa yoyote yatawangarimu watu wote walipa kodi bila kujali mkoa, chama, eneo lako...nk nk.

Jambo muhimu kabisa tunalopaswa kufahamu ni kuwa, hawa wafanyabiashara wanaokuja kwa jina la wawekezaji hawaji kwenye hizi nchi za Kiafrika ili kuzisaidia zipate maendeleo..la hasha, wanakuja kujichotea mali mbali mbali, hii imekuwepo toka enzi za ukoloni kwamba Afrika ni bara la kuchukua malighafi, lengo limebaki kuwa lilelile isipokuwa njia tu ni imebadilika, wakati zamani walitumia nguvu na "ujinga-ujima", sasa wanatumia "Ujinga mpya" kupitia mikataba mibovu, kupitia viongozi walafi na wala rushwa, kupitia watunga sheria ambao wengi ni wale wanaojua 3 K tu, hawa ukiwaambia hili ni jambo la chama watapitisha tu ..n.k.... Kiufupi ni kwamba, tofauti na zamani ambapo ukiwafukuza na ukawashinda kwa kutumia nguvu ilitosha kubaki na mali zako, kwa sasa kupitia mikataba mibovu, ukiivunja au kwenda kinyume na mikataba hiyo itakugharimu kwa kipindi kirefu sana.

Tukumbuke pia kwamba. mikataba hii ambayo ni siri ilishirikisha watu wachache sana akiwemo aliyekuwa mwanasheria mkuu "mzee wa vijisenti", Ndugu zangu, mkataba ambao umeidhinishwa na Mzee wa vijisenti ambaye alitanguliziwa share yake katika akaunti zake huko ughaibuni utakuwa una nini zaidi ya ujanja ujanja? Unaweza kuuvunja ukashinda? Penye rushwa weledi hukaa pembeni.

Tufanyeje kwa hapa tulipo?
Binafsi naamini katika win-win situation, viongozi wetu ni lazima wajenge mazingira ya kuaminiana na hawa wawekezaji, sio kukomoana kama hali alivyo sasa, tukumbuke hapa tunaongelea mikataba mibovu ambayo ina mianya mingi sana ya serikali kushindwa pindi tukifikia hatua ya kupelekana mahakamani.

Mwaka 1970, nchi ya Botwana iliingia mkataba wa uchimbaji wa Almasi na kampuni moja ya kigeni iitwayo De Beer, katika mkataba huo Botswana ilikuwa inapokea $20 Milion, kama Gawiwo kila mwaka. Lakini pamoja na hilo, Kampuni hii ilikuwa ikipata zaidi ya $60Milion kama faida, karibu mara tatu ya pesa ambayo serikali ya Botwasa ilikuwa inapokea...Nini serikali ya Botwana ilifanya? Je ilivunja mkataba? Hapana..Miaka 5 baadae mwaka 1975, serikali ilianzisha mchakato wa kuipitia upya mikataba na kujadiliana na kampuni ya De Beer hasa baada ya kugundulika maeneo mengine yenye madini, katika hili serikali ilifanikiwa kukubaliana na kampuni ile wafanye joint venture ya 50-50 kama kigezo ya kuendelea na mkataba wao, kutokana na majadiliano yaho kampuni iliridhia, na kutokana na hili, nchi ya Botwana ilipata maendeleo sana hasa kwa kuwa pesa nyingi zilielekezwa kwenye maendeleo ya nchi, na kutokana na hayo Botswana inatajwa kama miongoni wa nchi za Afrika ambazo rasilimali ya madini imewezesha nchi hiyo kuendelea.

Ni katika muktadha huo pia, naishauri serikali na watendaji wake wote wacool down, waache mihemko, waende chemba na kuanzisha majadiliano behind the door kupata better deal, Mikataba irudishwe mezani na majadiliano yafanyike, majadiliano bora huwezesha kuaminiana baina ya serikali na wawekezaji.

Ushauri unaweza kukubaliwa au kukataliwa

Wenu

Tume ya katika
 
Mikataba tatizo lakini kubwa linaloturudisha nyuma ni utendaji usiokuwa na utashi,weledi na uzalendo.

Mkaguzi wa TMAA na Wa TRA wakipewa mlungura wa 30 mil wasaini kilichokuwa declared na wenye migodi wao wanabonyea tuu.
 
Tatizo walikuwa wana declare uongo! Sasa nani amfuate mwenzake chemba?

Hapo inabidi sisi masikini ndio tumfuate muwekezaji tumshawishi tupitie upya mikataba hiyo. Wakati huohuo tuwataje watanzania wenzetu wote ikibidi hadharani kwa mikataba mibovu waliyotuingiza. Hapa namba moja ni Mkapa na namba 2 ni Kikwete.
 
Back
Top Bottom