Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,502
- 22,355
Jana kulikuwa na habari nzuri na ya kutia moyo kabisa kuhusu sera ya serikali kuhusu viwanda.
Mtanzania Mohammed Kiluwa anakuwa mtanzania wa kwanza kujenga kiwanda kikubwa cha nondo katika eneo la Disunyara lililoko Mlandizi mkoani Pwani.
Mohammed na kampuni yake ya Kiluwa Steel Group anashirikiana na wawekezaji wa kutoka Jamhuri ya watu wa China ambao wamekubali mawazo yake na mipango yake ya kujenga kiwanda hicho ambacho kitakamilika kwa awamu tatu ya kwanza ikiwa ni mwezi wa October mwaka huu, na kufuatiwa na kukamilika kwa amwamu ya pili mwezi February mwakani.
Kwa mujibu wa bwana Mohammed Kiluwa kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha tani 3000 za nondo na bidhaa zinazotokana na malighafi hiyo ya chuma na kuweza kuuza bidhaa hizo ndani na nje ya nchi hususan nchi jirani.
Kiwanda hicho kinatarajiwa kuiingizia serikali shilingi bilioni 200 ikiwa ni kodi na kuajiri wafanyakazi 500 ambao bila shaka watatoka katika maeneo ya mkoa huo.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa alitembelea kiwanda hicho jana na ameliagiza shirika la umeme la TANESCO kukamilisha uenezaji umeme katika eneo hilo ili kuhakikisha kiwanda hicho kinaenesha shughuli zake kwa ufanisi.
Kujengwa kwa kiwanda hicho ni muitikio wa watanzania wachache ambao wanathubutu kuja na mawazo ya kujenga kiwanda nchini Tanzania, ukizingatia kwamba ni watanzania wachache sana ambao wamefanya hivyo hadi sasa.
Kiwanda kingine kinachojengwa mkoani humo ambacho kinakarabia kukamilika na kinatarajiwa kutoa ajira 4500.
Kiwanda hicho kiitwacho Goodwill Ceramic kitakuwa kikitengeneza vigae kinajengwa katika kijiji cha Mkiu wilayani Mkutanga mkoani Pwani na kinatarajiwa kukamilika ujenzi wake mwezi December mwaka huu.
Akifafanua kuhusu kiwanda hicho mkurugenzi wake mkuu bwana Frank Young, amesema kiwanda hicho kitazingatia utoaji ajira kwa wananchi waliopo ndani ya eno hilo ambapo katika ajira 4500 ajira 1500 zitakuwa rasmi na 3000 zisizo rasmi.
Kiwanda hiki kitakapoanza kazi rasmi kinatarajiwa kuipatia serikali kiasi cha shilingi bilioni 30 kwa mwaka zikiwa ni mapato ya kodi.
Ni hatua ambayo inahitaji kupongezwa kwa nguvu zote na ya kutia moyo kuona kwamba sisi watanzania tunaweza kuja na mawazo kama ya mtanzania mwenzetu bwana Mohammed Kiluwa.
Ushauri wangu kwa serikali hii ya awamu ya tano ambayo imeahidi kutekeleza sera ya viwanda ni kuuwezesha mkoa wa Pwani kuwa kitovu cha viwanda kwa ukanda huu wa pwani.
Hiyo ni kutokana na kuwepo kwa miundombinu mbalimbali inayopita mkoani humo kama barabara na muungano wa barabara kama ya Bagamoyo na eneo kubwa la wazi mkoani humo ambalo linatosha kabisa kujenga viwanda vya aina mbalimbali.
Ni wakati sasa wa watanzania kutafuta wabia wa kutoka ndani au nje ya nchi na kujikita katika sekta hii muhimu katika kkuza uchumi wa nchi hususan ajira na makazi.
Tukumbuke kiwanda hicho kitatangeneza bidhaa mbalimbali zitakazotokana na chuma na hizo ni pamoja na mabomba ya maji, nondo za ujenzi na bidhaa zingine.
Si tu kuwepo kujengwa kwa viwanda katika eneo hilo bali pia shughuli zingine kama karakana kubwa, viwanda vya mbao, vipuri mbalimbali ambavyo vinategemea kwanda hicho ili kukamilisha bidhaa zingine na pia viwanda vya kusindika vyakula.
Aina ya viwanda vinavyoweza kujengwa mkoani Pwani:
Kiwanda cha kusindika vyakula,
Kiwanda cha mbolea ambayo inatokana takataka za majumbani za vyakula au kwa kiingereza "food waste recycling",
Kiwanda cha kutengeneza bidhaa zinazotokana na magazeti, maboksi na makaratasi,
Kuna aina mbalimbali za viwanda ambavyo vinaweza kabisa kuanzishwa na vijana bila kuwa na mitaji mikubwa na ni jukumu la serikali kupitia wakuu wa mikoa kujitahidi kutekeleza sera hiyo ya viwanda.
Huu ndio wakati wa kuwakusanya vijana mbalimbali ambao wamesomea fani mbalimbali na kuwasaidia kuanzisha viwanda na kujiajiri wenyewe, vijana hasa wa kutoka vyoni kama VETA na kwingine.
Hii iwe ni kampeni na kumshirikisha kila mtanzania afahamu kwamba bila kuja na wazo hauwezi kuendelea kufikia hatua ya kufanikiwa katika malengo yako iwe biashara au kujiajiri.
Ila mkoa wa Pwani sasa uwe ndio kitovu cha viwanda katika ukanda wa Pwani baada ya mkoa wa Dare-es-Salaam.