Vugu-Vugu
JF-Expert Member
- Feb 24, 2017
- 1,381
- 1,593
Kiongozi makini mara zote huzitazama fursa kama mtaji wa uhalali wake kama kiongozi.
Siku zote hufanya utafiti wa kina kabla ya kuamua jambo lolote analotaka kulifanya,
Nikupongeza Raisi wangu Dk John Joseph Pombe Magufuli kwa uthubutu wako wa-
kiwango cha juu kabisa achilia mbali ule wa MwL JK Nyerere uliomsaidia kupata uhuru
wa Tanganyika toka kwa Waingereza. Your running well but out of the ground.
Hapa nakumbuka maneno ya baba wa Taifa –Kiongozi bora awe na uwezo wa kugundua amekosea asahihishe-MwL JK Nyerere.
Hivi Mh Raisi alishajaribu kupitia takwimu ili kufahamu walau kati ya watu zaidi mil 52 waishio Tanzania Wangapi ni wakulima?Wangapi ni Wafanyakazi,Wangapi hawana kazi yeyote rasmi kama mimi,Walipa kodi ni wangapi? Leo naomba niongelee kundi moja tu la wakulima wenzangu.
Unapelekaje Tzs Trioni 2.24 kwenye kilimo sector yenye watu zaidi ya mil 35. Pamoja na bajeti hiyo ndogo bado Wizara ya Kilimo na Mifugo inapokea Tzs 1.7 trioni are we serious kweli kama serikali.
Hivi unaachaje sector ya kilimo yenye ajira zaidi ya mil 35 inayochangia asilia 32.4% ya pato la Taifa (GDP ) sawa na Tsh Trion 6.6 kwa kila mwaka, hizi hutokana na kilimo chenye bajeti ya Tr 1.7 Hebu fikiri kama tutawekeza hata nusu ya pato lake yaani Trioni 3.3. Tukanunua Matrecta,Plau,Pump za kumwagilia etc, Naamini Tutashangaza Dunia.
Hebu fikirini toka mazao ya biashara pekee Kilimo kinaliingizia Taifa zaidi ya US$ 1bn kil
mwaka. Kuna zaidi ya hekta mil 44 zinafaa kwa kilimo huku 33% sawa na hekta mil 14.52 pekee ndio zimetumika mpaka sasa kwa kilimo. Hivi mnajua kilimo ndio kila kitu Watanzania.
MAAJABU YA RELI PANA (standard gauge)
Napaata tabu kuelewa haya, japo watanzania wengi akili zetu zimejengwa kutumikia siasa zaidi kuliko Tanzania, Huwa nashangaa mtu anasapoti jambo hata kama ni la hovyo kiasi gani na halina maslahi kabisa kwa Taifa litapewa kiki kisa ni aliyetoa ni wa jamii yake/chama chake shame on us.
Itakumbukwa inchi kama South Africa pamoja na kuwa inchi ya kwanza Africa kwa Maendeleo yaani (Second World Country-Africa) lakini hawakufikia hapo kwa kuwa na ndege wala SGR .
Itakumbukwa FY 2013/2014, Shrika la reli SA liitwalo Passenger Rail Agency of SA (Prasa ) kwa mara ya kwanza ndio walitenga kiasi cha US$ 110bn sawa na Rand 1.5trion kwenye km 20,000 sawa US$0.0055bn/km yenye spidi ya 180-400km/h kwa kuwashirikisha Msumbiji na Botswana kwa kutumia umoja wao wa State Transport Company Transnet (SOC LTD) kuanza ujenzi wa network- Rail systm hiyo, lakini hii ni baada ya kuimarisha sana microsectors ikiwemo Kilimo na biashara.
Kwamujibu wa Gazeti la the The East African Waturuki /Wareno wanadai wameshinda tenda ya kutengeneza km 205 kwa US$ 1.215bn huku Prof Makame Mbarawa anasema ni US$187/300km.Hizo km 95 mkandarasi ni nani?
Hebu tujiulize ni kweli MORO-DAR ni km 300? Eti Mkurugenzi wa RAHCO anasema km 95 ni divergence na Stations yawezekanaje divergency railway ikawa ni nusu ya Mainrailway?
Jaribuni kufanya utafiti.Nijuavyo mimi Dar Moro ni km 190 pekee hizo km 15 ni za nani? AU ndio Sababu RAHCO-Reli asset Holding company wanatamani tubadili katiba ili Mh Dk Magufuli aendelee kutawala kwa ajili ya dili hizi? Hata hivyo kwanini Tanzania tulipe US$ 0.0059bn/km kwa reli yenye
Speed ya 160km/h juu kidogo ya wenzetu South Africa wenye SGR ya 400/km/h hapa hata mimi ningeombea Dk Magufuli atawale milele ile nipige dili lote kwenye km 2,561, Watanzania tuacheni ubinafsi.
Kwa mfano wenzetu wa Ethiopia walijenga SGR kutoka Ethiopia-Djibout km 750 kwa US$ 3.4 bn sawa na US$ 0.0045bn/km kwanini Tanzania km 215/1.215bn sawa na US$0.0059 bn/km. yaani kwa Mradi huo wa km 300 tutapoteza US$ 0.42bn kama tutafanya kwa km zote 2,561 tutapoza US$ 3.59bn hapa lazima watu waombee Rais Dk Magufuli atawale milele.
Maswali yangu kwa waziri mwenye dhamana Prof Makame Mbarawa
1. Iweje S.Africa wajenge SGR km 20,000 speed ( 180-400km/h) kwa US$ 110 bn= RD T1.5 bei sawa na Tanzania huku speed yetu ikiwa ni 160km/h
2. Iweje Etiopia wajenge SGR km 750 km speed (120-200 km/h)kwa US$ 3.4bn kwa bei juu kidogo ya Tanzania.
3. Wakati wa kusaini mkataba Prof Mbarawa aliwaambia Watanzania kuwa pesa ya Mradi itatoka kwa wafadhili na Serikalini, Lakini Raisi Magufuli anasema pesa yote ni ya serikali, Sasa watanzania tumwani nani? Na mnatudanganya ili iweje?-Gazeti la The citizen la 4/2/017
Nawatakia mapumziko mema ya siku kuu ya Pasaka.
Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake.