Ushauri: Nisomee kozi gani?

Ushauri: Nisomee kozi gani?

Korozoni

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2016
Posts
264
Reaction score
106
Habari wana JF


Naomba ushauri kutoka kwenu waungwana;

Nilimaliza kidato cha IV mwaka 2011 na kufanikiwa kupata alama ambazo ni za kawaida kama ifuatavyo:


Basic Mathematics-C

Chemistry-B

Engineering Science-C


Kiswahili-C

English Language-C


Civics-C

Geography-D


Surveying-C

Building Construction-D

Architectural Draughting-D



Ambayo ni Division II ya pointi 20

Na nikachaguliwa kwenda kidato cha V mwaka 2012 mchepuo wa PCM shule moja iliyokuwa na mchanganyiko wa O-level(Day) na A-level(Boarding).


Shule ilikuwa ndio inachukuwa A-level kwa mara ya kwanza na ilichukuwa wanafunzi wa michepuo ya Sayansi tupu ambayo ni PCB,CBG na PCM jambo la kusikitisha ilikuwa haina mwalimu wa A-level hata mmoja.

Na wanafunzi tulishauriwa na mkuu wa shule kwamba "Anayetaka kuhama Ruksa"

Na mimi nilikuwa sina mtu wa kunitafutia uhamisho nikaomba ruhusu ya wiki 2 na kuanza mchakato wa kutafuta shule,nilizunguka sana mpaka mkuu wa shule mojawapo akanihisi nimharifu na kutishia kuniitia Polisi kwa sababu namsumbua.Nilichanganyikiwa sana.

Nikasitisha kwa muda na kurudi shule lakini likizo ya mwezi Disemba mwaka 2012 nikaendelea kutafuta na mwishowe mwezi Februari 2013 nikapata nafasi kwenye shule nyingine nakupewa OPTIONS,
aidha nianze kusoma mwezi huo mpaka itakapoanza likizo ya muda mrefu kuhitimisha kidato cha V lakini kwa kulipa gharama zote za kidato cha tano ambayo ilikuwa kama 252,000 pamoja na michango au nijiunge muhula uliofuata mwezi Julai na kuanza kidato cha VI.

Kwa sababu sikuweza kumudu gharama hizo nikaomba kuchukua Option namba mbili.

Baada ya hapo nikarudi shuleni kupewa kibali cha kufuatilia uhamisho mkoani,mwishowe nikamaliza taratibu zote na muhula mpya ulipoanza nikahamia shule husika lakini walimu wa shule hiyo walikuwa wamemaliza kufundisha topics zote hivyo walikuwa wakifanya REVISIONS tu,hali ilikuwa mbaya kwa upande wangu lakini sikukata tamaa ingawa ilibaki miezi 10 kufanya mtihani wa Taifa.

Mwezi MEI mwaka 2014 nikafanya mtihani na sikufanikiwa kufaulu kwani nilipata alama hafifu kama ifuatavyo:

General Studies-D

Physics-D

Adv.Maths-E

Chemistry-E

Na mwaka huo ndio GPA ilianza kutumika,hivyo sikufanikiwa kwenda popote.


Na ilipotangazwa Diploma maalum ya Ualimu pale UDOM kipindi hicho nilikuwa natumikia Jeshi la Kujenga Taifa hivyo taarifa sikuzipata mpaka nilipomaliza mafunzo DISEMBA 2014 na kurudi mtaani.

Nikajaribu kukusanya pesa ili angalau niweze kurudia mtihani mwaka huu lakini gharama zake zilikuwa kubwa kwa sababu masomo yangu yanahitaji PRACTICALS,Gharama ya Kituo
niliambiwa 80,000,Mtihani 65,000.

Na topic nyingi za Sayansi ni gharama kubwa kwani zipo zinazofikia mpaka 45,000 na TOPIC zipo zaidi ya 20 hivyo nikagonga mwamba kwa mara nyingine.


Nimejaribu kutafuta vyuo vya afya nakutana na kigezo cha somo la BIOLOGY ambalo mimi nililisoma mpaka kidato cha pili tu kwa sababu ya Limit kwenye masomo ya kufanyia mtihani ambayo ni 10.

Sasa,naomba ushauri kwenu ni kozi ipi naweza kuichukua kwa vigezo hivyo vya ufaulu wa kidato cha nne;siku ambayo NACTE watafungua maombi.



Asanteni sana.
 
Civil engineering
Mechanical eng
Electrical eng
Geomatics
Quantity surveying
Architecture
Computer engineering
Land and mine surveying


OPT...
 
Civil engineering
Mechanical eng
Electrical eng
Geomatics
Quantity surveying
Architecture
Computer engineering
Land and mine surveying


OPT...
Soma laboratory technology ipo St John diploma lkn
 
Civil engineering
Mechanical eng
Electrical eng
Geomatics
Quantity surveying
Architecture
Computer engineering
Land and mine surveying


OPT...

Soma course yoyote kati ya hizi na hususani hizo mbili za juu. Huku kwingine utapata tabu sana mbeleni
 
Soma geomatics au geoinformatics ingawa ni ngumu Ila hutajuta zipo Ardhi university pale
 
Soma geomatics au geoinformatics ingawa ni ngumu Ila hutajuta zipo Ardhi university pale
Geomatics itamfaa zaidi hasa ukizingatia amesoma surveying O'level.

Anatakiwa aitafute Diploma kwanza kabla hajajiunga na ARU.
 
Macho yangu au
Screenshot_20190728-200308.jpeg
 
Back
Top Bottom