Ushauri: Nipo njia panda katika mahusiano yangu

Chilundumusi

New Member
Joined
Sep 27, 2018
Posts
1
Reaction score
1
Habari zenu za asabuh wakubwa na wadogo zangu.

Mimi ni kijana mwwnye umri wa miaka 26,ni mwanafunzi ambaye natarajia kumaliza chuo mwakan mungu akijalia.Kubwa na ambalo limenileta kwenu na kuja kuomba ushauri ni kwamba nmekuwa na mahusiano na binti mmoja ambaye tumeanza mahusiano yetu tangu mwaka 2011 ,huyu binti tulikutana mazngira flani enzi hizo ambazo bado tulikuwa na akili bado za kitoto tuliishi maisha flani hvi enzi hizo ambazo kila mmoja wetu imebaki kwenye memory yake.

Kutokana na mambo ya shule mm nlibahatika kutoka mazingira yale ambapo nilimuacha mpweke na kama mnavyojua Mara nyingi mahusiano ya mbali huvunjika kusema kwl kuna kipindi kama mnavyojua ujana nliingia kwenye mahusiano na wasichana wengine hvyo nikaachana nae ingawa binti nlimuumiza sana,,maisha yaliendlea ,sasa mwaka Jana kama mungu binti alinitafuta kupitia fb kwan nlibadilisha namba ,kilichopelekea mpka anitafute aliniambia kuwa kuna siku alkuwa ofcn(ameajiliwa ofc moja mjini Zanzibar) kuna kijana alipita ofcn hapo ambae anasema tunafanana kila kitu,anasema kupitia hiyo picha ilimpelekea kunitafuta.

Baada ya kunitafuta nilimuelezea maisha yote ya kimahusiano nliyoyapitia na malengo niliyonayo kwa sasa kuhusu mahusiano ambapo nilimuomba turudiane ili baadae ambapo 2020 tuoane, alnikubalia tukaendleza mahusiano yetu mpka sasa,kusema kwl huyu mschana amekuwa na upendo wa kwl kwangu kama mnavyojua maisha ya shule amekuwa akinisaidia sana vihela vya hapa na pale vile vile amekuwa akinisikiliza na kunionyesha upendo haijalishi nipo ktk hali gan,hajabadilika toka kipindi kile tulipoachana mpka Leo hajabadilika kitabia kwan huyu binti kinachomsaidia ni mcha mungu hilo nalitambua toka kipindi tulichokua wote.

Changamoto iliyopo na ambayo imenifanya nije kwenu kuomba ushauri ni kwamba mm mwakani namaliza chuo mwezi kama wa nane ambapo tena nitakuwa na mwaka mmoja wa Internship(mafunzo kwa vitendo )nilimwambia huyo mpenzi wangu awaambie wazazi wake ili na mm mwakani by mwez wa tano nianze kufanya michakato ya kutoa posa na mambo mengine,sasa huyu mpenzi wangu Jana ameongea na wazazi wake wamekataa kisa dini zetu kwan mm ni mkatoliki(RC)na yy ni mlokole,wazazi wake ni wachungaji hivyo wamemwambia kuwa atawaahibisha ,kwa upande wa binti yupo tayar kubadilisha na kunifuata mm hvyo binti yupo njia panda maana amesema wazazi wake wameongea sana na wamemwambia akibadili dini atambue kuwa wale sio wazazi wake.Hivyo wakubwa na wadogo zangu nipo njia panda kwan binti nampenda na anafaa kwl kuwa wife material na mm kubadili dini na kumfuata ni ngumu hivyo nipo njia panda na nmekuja kwenu wakubwa zangu na wadogo zangu kuomba ushauri wenu.

Mungu awabariki
 
Badili dini ujiunge na hao walokole ili umpate huyu binti mlokole. Si kitu rahisi tu?? We nenda kwa walokole ili wazazi wake wawe kweli ndio hao. Hapo njia panda ni wapi?? Kupenda umependa wewe, tena umeshahakiki kuwa binti ni wife material sasa unataka nini?? Tukuambie usioe??
 
Badili dini ww,,,
Ukipenda boga penda na usifikirie lake
 
duuuu mbona hizi dini tumeletewa aise alafu huku afrika zinatupeleka puta hivi chukua Mchumba huyo Mkuu.
 
kwani wote ni din moja mathehebu tu ndio tafauti achana nae tafuta mwingine
 
Habari zenu za asabuh wakubwa na wadogo zangu.

Mimi ni kijana mwwnye umri wa miaka 26,ni mwanafunzi ambaye natarajia kumaliza chuo mwakan mungu akijalia.Kubwa na ambalo limenileta kwenu na kuja kuomba ushauri ni kwamba nmekuwa na mahusiano na binti mmoja ambaye tumeanza mahusiano yetu tangu mwaka 2011 ,huyu binti tulikutana mazngira flani enzi hizo ambazo bado tulikuwa na akili bado za kitoto tuliishi maisha flani hvi enzi hizo ambazo kila mmoja wetu imebaki kwenye memory yake.

Kutokana na mambo ya shule mm nlibahatika kutoka mazingira yale ambapo nilimuacha mpweke na kama mnavyojua Mara nyingi mahusiano ya mbali huvunjika kusema kwl kuna kipindi kama mnavyojua ujana nliingia kwenye mahusiano na wasichana wengine hvyo nikaachana nae ingawa binti nlimuumiza sana,,maisha yaliendlea ,sasa mwaka Jana kama mungu binti alinitafuta kupitia fb kwan nlibadilisha namba ,kilichopelekea mpka anitafute aliniambia kuwa kuna siku alkuwa ofcn(ameajiliwa ofc moja mjini Zanzibar) kuna kijana alipita ofcn hapo ambae anasema tunafanana kila kitu,anasema kupitia hiyo picha ilimpelekea kunitafuta.

Baada ya kunitafuta nilimuelezea maisha yote ya kimahusiano nliyoyapitia na malengo niliyonayo kwa sasa kuhusu mahusiano ambapo nilimuomba turudiane ili baadae ambapo 2020 tuoane, alnikubalia tukaendleza mahusiano yetu mpka sasa,kusema kwl huyu mschana amekuwa na upendo wa kwl kwangu kama mnavyojua maisha ya shule amekuwa akinisaidia sana vihela vya hapa na pale vile vile amekuwa akinisikiliza na kunionyesha upendo haijalishi nipo ktk hali gan,hajabadilika toka kipindi kile tulipoachana mpka Leo hajabadilika kitabia kwan huyu binti kinachomsaidia ni mcha mungu hilo nalitambua toka kipindi tulichokua wote.

Changamoto iliyopo na ambayo imenifanya nije kwenu kuomba ushauri ni kwamba mm mwakani namaliza chuo mwezi kama wa nane ambapo tena nitakuwa na mwaka mmoja wa Internship(mafunzo kwa vitendo )nilimwambia huyo mpenzi wangu awaambie wazazi wake ili na mm mwakani by mwez wa tano nianze kufanya michakato ya kutoa posa na mambo mengine,sasa huyu mpenzi wangu Jana ameongea na wazazi wake wamekataa kisa dini zetu kwan mm ni mkatoliki(RC)na yy ni mlokole,wazazi wake ni wachungaji hivyo wamemwambia kuwa atawaahibisha ,kwa upande wa binti yupo tayar kubadilisha na kunifuata mm hvyo binti yupo njia panda maana amesema wazazi wake wameongea sana na wamemwambia akibadili dini atambue kuwa wale sio wazazi wake.Hivyo wakubwa na wadogo zangu nipo njia panda kwan binti nampenda na anafaa kwl kuwa wife material na mm kubadili dini na kumfuata ni ngumu hivyo nipo njia panda na nmekuja kwenu wakubwa zangu na wadogo zangu kuomba ushauri wenu.

Mungu awabariki
Badili tu kwani dini si ndo hiyo hiyo ,tofauti ni dhehebu tu
 
Usimuoe ila mfanye awe mchepuko wako wakudumu,tafuta mwingine oa.Hatakulaumu kwasababu yeye anajua sababu zako.
 
hivi kumbe wafia dini bado wapo pole mkuu kama naona ulichifanya Mara ya kwanza kinaenda kurudi upande wako....time will tell
 
Unachezea bahati kwa mara ya pili yaani unataka kuacha wife material kisa dini! Badili uoe huyo mke naamini hutajuta maana ukibadili dini bado wote mnaamini ktk YESU KRISTO tofauti ni kuwa nyie mnapata sakrament wao hawapati, mna Padr wao wana Mch. nk. Badili dini ili Uoe, ukishaoa kwa upande wa kanisani mkiwa kwako mnazama Roma kwani mtaishi na wazazi wake kwamba watawaona mnaenda Roma.

Hizi takataka tumeletewa, zitatukosesha wife material wengi.
 
Bado sijaamini ulichokiandika, halafu kuna tofauti kati ya dhehebu na dini jua tofauti kwanza ndo utake ushauri
 
Halafu Hapo tatizo sio Dini Tatizo ni dhehebu mm nikajua demu Muislam kumbe mlokole? Mbona Barida tuu unaenda kilokole mpaka siku ya ndoa ila mkubaliane na mkeo baada ya ndoa kila mtu anarudi kanisani kwake
 
mtie mimba ndo watajua aibu au la,mambo ya kubaguana hayo yashapitwa
 
Endeleeni na mapenzi yenu.. Wakimkataa saivi badaae watamurudia tu. Ukimaliza Chuo Tia Mimba afu tulia.
 
Tatizo dogo sana hilo me nilizani dini ndio tofauti kumbe madhehebu2
 
Hata ukibadili dini ila Mungu ni huyo huyo mmoja so haina madhara cha msingi matendo yako yawe ya kumpendeza Mungu na mkeo mtarajiwa kijana wangu
 
Upo njia panda unaelekea wapi? Si uchukue usafiri mwingine kama vile mjaze mimba tu, uone kama hawajakukabidhi fasta.
 
ushauri wa kibingwa
ongea na watu wa kwenu waambie kuwa unapretend tu kuwa unaenda ulokole ili ufunge ndoa pia hata hao wakwe zako wadanganye hivyohivyo

ukishapata jiko endelea na RC yako yeye atabaki na ulokole wake madhehebu yasiwe kikwazo kwenye malengo yenu...

kwani hao wakwe mtakuwa mnakaa nao au..? kama hamtakuwa mnakaa nao basi ww pretend tu kwa hayo masaa mawili ya ndoa then maisha yaendelee

USHAURI WA KIBINGWA nakwambia hivyo maana nimeshashuhudia binamu yangu akipretend kusilimu dini ili tu apate jiko

sababu nyumbani kwa mwanamke walitishia kumtenga kama akislimu kuwa mkristo na wao walikuwa wanapenda sana na tayar wana malengo yao

baada ya ndoa kila mmoja akaendelea na dini yake ila ikawa siri yao

wazazi wa mwanamke hadi kesho wanajua yule binamu yangu bado ni muislamu... na ndoa yao ipo vizuri tu na maisha yanaendelea

Maisha ni mipango tu kujifanya mlokole masaa mawili haufi broo
 
Back
Top Bottom