Tafuta eneo lenye chanzo cha maji, nunua pump yako na mpira, anzisha kilimo cha mbogamboga.. lima eneo kama nusua eka tu kwa kuanzia..lima chunese, michicha, sukuma wiki, mnavu, carotte, hoho, nyanya kiasi na pilipili mbuzi..uwe na kijana wako mmoja tu. Unaenda sokoni unachukua order za wamama wale wauza mboga wanakuwa wanakuja kununua kwako. Trust me, hadi ualize kunyeshea nusua eka jioni muda nao utakuwa umesogea.. hapo utashangaa mwenyewe utakavyoingiza kipato cha ziada. hapo masuala ya vyeti vyako vya degree weka pembeni.. ni kazi ya mikono na pia ni zoezi.. huna haja ya kwenda kupotezea nguvu zako gym..unafanya zoezi hapo hapo unatengeneza kipato.