queen me
Member
- May 4, 2017
- 41
- 17
Habari wana JF,
Napenda kuchukua fursa hii kuleta yanayonisibu ili nijue muafaka wa hili. Siyo kwamba mimi ni mgeni JF, hapana. Nimelazimika kuja na ID mpya kwa sababu ya zamani kuna marafiki wengi wanaijua.
Nije kwenye mada.
Mimi ni dada. Nina miaka 28. Naishi Arusha ila Arusha siyo nyumbani kabisa. Natokea katika kijiji A. Kuna dada yangu anaishi Arusha. Nilipomaliza elimu ya msingi aliniita nikakae naye pamoja na kujiendeleza kielimu. Na kweli nilienda na nikajiendeleza kielimu.
Kipindi hicho wakati nasoma sekondari kuna ndugu wa mume wa daday angu alikuja naye pale nyunbani kwa dada, ni mtoto wa shangazi yake na mume wa dada angu. Kwa hiyo shemeji yangu anawita binamu.
Kadri siku zilivyokuwa zinaenda mazoea kati yangu mimi na mdogo wa shemeji yangu yaliongezeka.Tumwite (Bry ) ili tuelewe vyema. Tukawa tunasoma wote, discussion wote, tukajikuta tunapendana na Bry, ila tulijipangia kwamba hamna kujihusisha na mapenzi mpaka tumalize shule. Kweli tulifanikiwa. Tulipendana sana.
Ilikuwa kwa siri sana ila baadaye ndugu walikuja kugundua mahusiano yetu. Hapo ndo balaa lilipoanza. Ndugu zangu hawataki niwe na mahusiano na Bry kwa kusema ni mkosi mkubwa, na Bry ananipenda sana sana na yupo tayari kugombana na watu kwa ajili ya penzi letu.
Pia Bry nilikuja kugundua yeye ni mdogo nimemzidi miaka mitatu. Nilipogundua hilo nilimsihi tuachane kwani yeye ni mdogo. Hajakubali na mimi kila nikimwambia umri wangu umeshaenda nahitaji kuwa na familia kwa sasa, hataki anadai anatafuta kazi ili tuzae na mtoto wetu. Na mimi sijawahi kuwa na mahusiano pembeni hata siku moja. Nampenda.
Ila kila nikifikiria ndugu wanavyopiga vita nakuwa sijui hatima ya haya mapenzi, na nikimuangalia Bry bado hajajipanga kimaisha kwani bado anategemea wazazi. Naona mimi umri wangu umeenda sana, kumpenda nampenda ila ndo vikwazo na umri.
Naombeni kufahamu kama kuna tatizo mimi kuoana na Bry ambaye ni binamu na shemeji yangu, mume wa dada angu, na kama ni mkosi.
NB: Haya ni maisha yangu halisi nimeishi na ni kweli kabisa. Sio Story ya kutunga.
Msaada wenu. Sielewi hata nifanye nini.