Kwa kweli niliposoma hiyo story hata mimi nimeshangaa, kati ya magonjwa ambayo mtu hawezi kuyaficha kwa mtu unayeonana naye mara kwa mara ni Sickle Cell...lazima ungejua kuwa ni mgonjwa! Labda kama ana Sickle Cell trait, ambayo mbebaji wa trait si lazima awe na dalili. Sickle Cell kama ugonjwa haisababishi kuogopa..lakini muathirika wa huo ugonjwa kuna uwezekano mkubwa wa kuapata athari za kisaikolojia akawa muoga na kutumia uongo kujilinda. Japo sioni link kati ya uongo wake na ugonjwa huo...Wagonjwa wa Sickle Cell huudhuria clinic maalum kila mwezi, muombe uende naye siku yake ya clinic utaujua ukweli.