USHAURI :Nimepata kazi nikiwa bado nasoma

mindsett

Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
35
Reaction score
7
habari wakuu. naomba ushauri kuhusu kazi niliyopata.

Kwanza niseme nashukuru Mungu nimepata kazi halmashauri moja katika mkoa mmoja(jina nahifadhi), niliomba kazi kwa kutumia cheti cha diploma na wakati huo nikiwa nasoma masomo ya jioni taasisi moja hapa DSM . Kazi niliyoomba kituo cha kazi kilikuwa DSM hivyo niliamini nikipata nitaweza kuendelea kusoma jioni ili nimalizie masomo yangu ambapo kwasasa nipo mwaka wa tatu na wa mwisho nategemea kumaliza chuo mwezi july mwakani .

Lakini kwabahati mbaya/nzuri sikupata kazi ya kwanza na nikuridhika kukosa kwa wakatihuo wa october mwaka huu hadi wiki iliyopita nilipoona nimeitwa na kupangiwa kazi mkoa mmoja unaopakana na tabora .

Kwasababu ninapata mkopo wa bodi unaonisaidia ktk elimu ili mshahara niliokuwa napata ukinisaidia kuhudumia familia kwasasa nina familia na watoto wawili na mtoto wa pili ndio kwanza ni mchanga wa umri wa mwezi.

Naomba ushauri kwamba nisitishe masomo ? na nikiwaza kuhusu kusitisha naona uwezekano wa kupata mkopo tena kwa baadae itakuwa ngumu hivyo nitasoma kwa shida. wakati huohuo nipo kwenye ujenzi wa nyumba kwa hapa dsm na inakuwa ngumu kuhama na familia haraka kwasababu wife nae anajiandaa kuanza masomo ktk chuo kimoja hapa dsm hapo baadae mwakani
Tatizo langu sio eneo la kaz nipo radhi kufanya kaz popote tatizo n kuingiliana kwa mambo ambayo yaweza kunichelewesha kufikia malengo kwakuzingatia bado nahitaji kusoma zaidi hata baada ya kuhitimu degree na niliomba kazi baada ya kukosa uhakika wa ku renew mkataba kwenye taasisi binafsi ambayo mwezi DEC ndio mwisho wa mkataba japokua wako tayari niingie mkataba mwingine wa miaka mitatu .

Natakiwa kuripoti ndani ya siku 14 kuanzia juzi masomo yanaendelea tuna wiki ya tatu toka tufungue chuo .
kwakweli nipo kwenye wakati mgumu wa kufanya maamuzi sahihi ili nimalizie masomo pia nisome kwasababu sijui kama mkurugenzi ninaemkuta atakubali nirudi kumalizia masomo kwa miezi michache iliyobaki.

ushauri wako ni wa muhimu kwa wakati huu nilionao .
Natanguliza shukrani .
 
Option nzuri sitisha masomo kwa mwaka mmoja then nenda kazini alafu utaomba nafasi ya kumalizia muda uliobaki
 
Kwa upande we maslahi hapo ulipo sasa na hili halmashauri wapi pako vzr zaidi!?

Fanya uchambuzi wa kina wewe binafsi pia ushauri wa humu ukusaidie tu kulingana na yale uliyoyapata.....
 
je nikisitisha masomo uwezekano wa kupata mkopo tena upo ? maana kujilipia mm na mwenzi kwa wakati mmoja ni ngumu bila mm kupata mkopo ili salary yangu imsaidie nayeye kusoma chuo maana itafika muda watoto itakuwa zamu yao kusoma na sio sisi tena
 
habari wakuu. naomba ushauri kuhusu kazi niliyopata.

Kwanza niseme nashukuru Mungu nimepata kazi halmashauri moja katika mkoa mmoja(jina nahifadhi), niliomba kazi kwa kutumia cheti cha diploma na wakati huo nikiwa nasoma masomo ya jioni taasisi moja hapa DSM . Kazi niliyoomba kituo cha kazi kilikuwa DSM hivyo niliamini nikipata nitaweza kuendelea kusoma jioni ili nimalizie masomo yangu ambapo kwasasa nipo mwaka wa tatu na wa mwisho nategemea kumaliza chuo mwezi july mwakani .

Lakini kwabahati mbaya/nzuri sikupata kazi ya kwanza na nikuridhika kukosa kwa wakatihuo wa october mwaka huu hadi wiki iliyopita nilipoona nimeitwa na kupangiwa kazi mkoa mmoja unaopakana na tabora .

Kwasababu ninapata mkopo wa bodi unaonisaidia ktk elimu ili mshahara niliokuwa napata ukinisaidia kuhudumia familia kwasasa nina familia na watoto wawili na mtoto wa pili ndio kwanza ni mchanga wa umri wa mwezi.

Naomba ushauri kwamba nisitishe masomo ? na nikiwaza kuhusu kusitisha naona uwezekano wa kupata mkopo tena kwa baadae itakuwa ngumu hivyo nitasoma kwa shida. wakati huohuo nipo kwenye ujenzi wa nyumba kwa hapa dsm na inakuwa ngumu kuhama na familia haraka kwasababu wife nae anajiandaa kuanza masomo ktk chuo kimoja hapa dsm hapo baadae mwakani
Tatizo langu sio eneo la kaz nipo radhi kufanya kaz popote tatizo n kuingiliana kwa mambo ambayo yaweza kunichelewesha kufikia malengo kwakuzingatia bado nahitaji kusoma zaidi hata baada ya kuhitimu degree na niliomba kazi baada ya kukosa uhakika wa ku renew mkataba kwenye taasisi binafsi ambayo mwezi DEC ndio mwisho wa mkataba japokua wako tayari niingie mkataba mwingine wa miaka mitatu .

Natakiwa kuripoti ndani ya siku 14 kuanzia juzi masomo yanaendelea tuna wiki ya tatu toka tufungue chuo .
kwakweli nipo kwenye wakati mgumu wa kufanya maamuzi sahihi ili nimalizie masomo pia nisome kwasababu sijui kama mkurugenzi ninaemkuta atakubali nirudi kumalizia masomo kwa miezi michache iliyobaki.

ushauri wako ni wa muhimu kwa wakati huu nilionao .
Natanguliza shukrani .

Mkuu nenda kwanza ulipopangiwa ukifika ongea na mkurugenzi wako aliekuajiri

mueleze kila kitu hali halisi baada ya hapo utamskia atakachokuambia akikubali usome sawa itakuwa vizuri huku nafasi yako ya ajira ikiwepo

but akikataa sasa usisome nakushauli nenda chuoni ongea na mkuu wako wa department na utawala kwa ujumla ili usitishe masomo kwa huo mwaka mmoja namaanisha( ku postpone mwaka)

ili.badae.ukipata nafasi ukaendelee pale ulipoishia ktk huo mwaka

Kuhusu mkopo wako.pia unaenda bodi ya mkopo pale mwenge na wenyewe unaenda ku suspend yani unakuwa suspended kwa huo mwaka unaotaka wala hawana shida ndugu yangu utaendelea kutolewa pale tu utakapotaka kusoma tena so ni wewe tu kuamua ktk hayo niliyokushauli
 
kazi zenyewe za kusimamiwa na Mh magufuri huko serikalini utaweza kweli?, kama umejipima nenda huko serikalini japo najua utaratibu za zamani unaweza ukaisha muda si mrefu
 
Endelea na masomo tu hiyo nafasi iachie tu Mungu yu nawe utamaliza chuo na kupata nafasi nyingine
 
Kaka mimi nimmoja wapo ya watu waliopangiwa kazi utumishi tena halmashauri post ya assistant accountant nimeenda kulipoti na nimemuomba mkurungenzi ruksa ya kwenda kusoma nimeruhusiwa so nenda bro kazi serikalini zinasumbuwa!!!
 
nashukuru wote kwa ushauri wenu mnanisaidia kufanya maamuz sahihi . mr bwai nita ku pm please .
 
Nakushauri kama unaona KAZI hiyo inalipa ailisha mwala,mkopo kitu gani bwana,jali future yako kama unaona maisha yako yanajali sana ajira.
 
je nikisitisha masomo uwezekano wa kupata mkopo tena upo ? maana kujilipia mm na mwenzi kwa wakati mmoja ni ngumu bila mm kupata mkopo ili salary yangu imsaidie nayeye kusoma chuo maana itafika muda watoto itakuwa zamu yao kusoma na sio sisi tena

Kama upo mwaka wa mwisho malizia masomo yako kwa amani,
Mungu ataleta kheir utapata kazi ingine tena nzuri zaidi ya hiyo.
 
Mwaka mmoja tu kuairisha siyo ishu coz najua hapo ni lazima upige KAZI mwaka miwili mitatu ndiyo urudi kusoma.Acha woga.Woga utakucost,wengi wanajuta.Kusoma mwaka mmoja si ishu unamalizia tu!
 
Nenda kwa mkuruguzenze..mwambie ukweli..pia ata ukisitisha mwaka huu ukasoma..hauwezi kushindwa kujilipia muhula mmoja uliobaki
 
Kijana shule muhim, maliza hiyo Shule then utafute kazi, ila ungerenew huo mkataba ingekuwa bomba zaidi!
 
habari wakuu. naomba ushauri kuhusu kazi niliyopata.

Kwanza niseme nashukuru Mungu nimepata kazi halmashauri moja katika mkoa mmoja(jina nahifadhi), niliomba kazi kwa kutumia cheti cha diploma na wakati huo nikiwa nasoma masomo ya jioni taasisi moja hapa DSM . Kazi niliyoomba kituo cha kazi kilikuwa DSM hivyo niliamini nikipata nitaweza kuendelea kusoma jioni ili nimalizie masomo yangu ambapo kwasasa nipo mwaka wa tatu na wa mwisho nategemea kumaliza chuo mwezi july mwakani .

Lakini kwabahati mbaya/nzuri sikupata kazi ya kwanza na nikuridhika kukosa kwa wakatihuo wa october mwaka huu hadi wiki iliyopita nilipoona nimeitwa na kupangiwa kazi mkoa mmoja unaopakana na tabora .

Kwasababu ninapata mkopo wa bodi unaonisaidia ktk elimu ili mshahara niliokuwa napata ukinisaidia kuhudumia familia kwasasa nina familia na watoto wawili na mtoto wa pili ndio kwanza ni mchanga wa umri wa mwezi.

Naomba ushauri kwamba nisitishe masomo ? na nikiwaza kuhusu kusitisha naona uwezekano wa kupata mkopo tena kwa baadae itakuwa ngumu hivyo nitasoma kwa shida. wakati huohuo nipo kwenye ujenzi wa nyumba kwa hapa dsm na inakuwa ngumu kuhama na familia haraka kwasababu wife nae anajiandaa kuanza masomo ktk chuo kimoja hapa dsm hapo baadae mwakani
Tatizo langu sio eneo la kaz nipo radhi kufanya kaz popote tatizo n kuingiliana kwa mambo ambayo yaweza kunichelewesha kufikia malengo kwakuzingatia bado nahitaji kusoma zaidi hata baada ya kuhitimu degree na niliomba kazi baada ya kukosa uhakika wa ku renew mkataba kwenye taasisi binafsi ambayo mwezi DEC ndio mwisho wa mkataba japokua wako tayari niingie mkataba mwingine wa miaka mitatu .

Natakiwa kuripoti ndani ya siku 14 kuanzia juzi masomo yanaendelea tuna wiki ya tatu toka tufungue chuo .
kwakweli nipo kwenye wakati mgumu wa kufanya maamuzi sahihi ili nimalizie masomo pia nisome kwasababu sijui kama mkurugenzi ninaemkuta atakubali nirudi kumalizia masomo kwa miezi michache iliyobaki.

ushauri wako ni wa muhimu kwa wakati huu nilionao .
Natanguliza shukrani .
Mkuu hapo ni rahisi sana nenda kareport then uombe ruhusa ya kumalizia chuo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom