Ushauri- ndoa inataka kuvunjika huku

Dunia imekuwa ya ajabu Sana ndugu yako anasaidiwa na mume wako mke anaksirika anataka kuvunja ndoa.? Hivi wanawake KWA nn hawapendani kiasi hiki?? Lakin kwenye shughuli wanajifanya ndugu wanavaa sare
 
Mke atalaumiwa bure!
Jamaa anatumia Mali za familia kwa Faida binafsi.

Mke kashtukia muwewe anaogolea ndani kwa ndani.
 
Hapana mkuu, jamaa ni mtu na heshima zake tu, anajiheshimu Sana na anampenda Sana tu mkewe. Hata chumba cha shemeji yake huwa hana mazowea ya kuingia.
Hata shemeji yake huwa anakuwa Kama anakauoga hivi kwa huyo mume wa dada yake.
 
Mwanzoni alimshirikisha ndio akaja kumwambia mkewe na mkewe akamshukuru kwa moyo wake wa upendo aliouonyesha, hii ya sasa ameenda amelipa mkewe amempa tu taarifa tayari ameshamlipia shemeji yake miezi 6 mke akapanic
 
kesi hiyo kifupi huyo jamaa amezingua hakumshirikisha mkewe juu ya msaada kwa mdogo wake, cha kufanya apeleke kesi kwa hao wazazi wa ndugu wa kike watasameheana tu.
Jamaa amemlipia shemeji yake then akamjulisha mkewe mke akapanic.
Asante kwa ushauri wako mkuu nitauwakilisha
 
Kiini cha huo mgogoro sasa ni nini?? Mke ana madai gani ya ziada?
Mke kanuna anadai ataondoka ampishe mdogo wake aje akae na jamaa, amepanic vibaya Sana, anasema inakuwaje misaada inazidi kwa mdogo wake?
Ushauri wako mkuu.
 
Mwanzoni alimshirikisha ndio akaja kumwambia mkewe na mkewe akamshukuru kwa moyo wake wa upendo aliouonyesha, hii ya sasa ameenda amelipa mkewe amempa tu taarifa tayari ameshamlipia shemeji yake miezi 6 mke akapanic
Ndo nimekwambia alivyoenda kulipa bila kushauriana na mkewe tayari ilikuwa siri. Siri aliifichua baada ya kumwambia mkewe.
Unadhani kwann mkewe kakasirika?
Angeambiwa kabla ya kodi kulipwa angekasirika?

Jiulize haya maswali halafu utamuelewa mke wake:
Walikutana saa ngapi kuongelea kuwa kodi imefikia?

Wakakutana saa ngapi kupeana pesa?

Mazungumzo kuwa ilipwe ya miezi sita yalifanyikia wapi na kwa mtindo gani?

Usisahau kuwa dada mtu anamuelewa mdogo mtu na tabia zake vizuri.

JAMAA AKAE CHINI NA MKE WAKE AMWAMBIE ALITELEZA KUTOKUMUULIZA KABLA HAJALIPA NA ALIFIKIRI MDOGO MTU WALISHAONGEA NDO MAANA AKAJA KWAKE KISHA AACHE HUO UJINGA.
 
Hapana mkuu, jamaa ni mtu na heshima zake tu, anajiheshimu Sana na anampenda Sana tu mkewe. Hata chumba cha shemeji yake huwa hana mazowea ya kuingia.
Hata shemeji yake huwa anakuwa Kama anakauoga hivi kwa huyo mume wa dada yake.
basi kuna kawivu ka dada mtu kwa mdogo wake huwenda kazidiwa sura na vitu vingine, hebu aache kulipa kodi na wengine tukasaidie,
km kweli shemeji halipi hebu mwaacheni km hatalipa,
 
Sawa mkuu, Asante kwa ushauri wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…