*Unajenga wapi/mkoa gani?
*Una kiwanja, kipo katika hali gani? Kipo kwenye mwinuko au flat? Ardhi ya eneo hilo ikoje? Ni udongo wa aina gani?
*Je, vifaa vya ujenzi katika eneo hilo vinauzwa bei gani? ie. Mchanga, tofali, kokoto, maji, cement, vifusi, mbao.
*Ufundi katika eneo hilo unagharimu kiasi gani? Umekutana na mafundi wangapi kusikiliza bei zao, umehakiki baadhi ya kazi zao?
*Una mchoro, umechorewa na wataalamu, wamefika kuangalia jinsi eneo lilivyo? Au umenunua mchoro blindly?
Maoni: Kama una mchoro, tafuta fundi, elewana nae bei ya ufundi, then yeye ndio atakupa makadirio ya tofali, mchanga, mbao, maji, nk kutokana na ukubwa wa nyumba unayotaka kujenga.