Ushauri mzito kwa wasaidizi wa rais Magufuli

NYARUKURURU

JF-Expert Member
Aug 22, 2016
349
199
USHAURI WA BURE NA WA MUHIMU SANA KWA WASAIDIZI WOTE WA MH, RAIS DR. JOHN POMBE MAGUFULI NDANI YA CHAMA NA SERIKALI


Ikiwa imebaki takribani mwezi mmoja kusherekea miaka 40 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi Nimeamua kuandika makala hii ili kuwa shauri viongozi wa ngazi zote wa chama na Serikali yake ili waweze "KUJISAHIHISHA "katika mambo yasiyofaa wayatendayo.

Chama cha Mapinduzi ni chama ambacho kinawapa fursa wanachama wake kukosoa jambo lolote lile linalokwenda kinyume na katiba, kanuni na maadili ya Chama hicho na ni tofauti na vyama vya upinzani ambavyo ukikosoa jambo ndani ya chama unaitwa msaliti na kuvuliwa uanachama.

Ndugu wasomaji wangu katika Makala yangu hii yakupasa kuisoma kwa umakini na uvumilivu kwani ni ndefu na inayochambua vitu kwa mifano dhahiri pasipo kuonea haya jambo lolote, mtu yeyote au taasisi yeyote na lengo ni kuwekana sawa kwa maendeleo ya nchi yetu sote bila kujali Itikadi zetu.

Kwanza, nianze kwakuwapongeza mawaziri wote wanaofanya kazi chini ya Mh, JPM, makamu wa Rais na waziri wetu mkuu kwa kazi nzuri sana wanayoifanya hakika Mungu awalinde sana na awape hekima zaidi.

Japo hapo juu nimewapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya, wapo baadhi ya mawaziri wachache hawafanyi kazi yao kisawasawa inavyotakika na ndo leo ninaenda kuwakosoa ili wajisahihishe nina imani hata Mh, Rais atakuwa anawashangaa kwa jinsi mnavyo muangusha ila ipo siku atakuja kuwambia au kuwachukulia hatua, mimi nimeamua kuwasema mapema ili mfanye kazi ya wananchi mliotumwa.

Kuna waziri mmoja ni mtaalamu wa kuongea jukwaani na kupanga mikakati lkn tangu apewe wizara yuko kimya kanakwamba kasafiri, wakati Si kawaida yake, wananchi wanajiuliza huyu Mh, alipewa wizara asiyoitaka? Kwanini hafanyi kazi? lkn mpaka sasa majibu hakuna, kwani Kuna wizara nzuri kuliko nyingine? Mh, waziri najua unajifahamu uonapo makala hii JISAHIHISHE, kafanye kazi Kama ulivyokuwa awamu ya nne, kipindi kile ulikuwa Naibu waziri mzuri mno na ulifanya kazi zaidi ya waziri.

Pia, Kuna Mh, waziri mmoja unakera watu wewe muda wote ni kampeni badala ya kuwafanyia wananchi kazi uliotumwa na Mh, Rais, makamu wa Rais na waziri mkuu. Kuna tabia yako moja ya kila unachokifanya lazima ujipige picha na kuturushia kwenye magroup, sisi wananchi tunajua Kama wewe ni mwajibikaji tutaona tu hakuna haja ya kutuaminisha.

Wewe Mh, waziri fanya kazi acha maandalizi ya kuwa Rais mwaka 2025, jifunze kwa Mh, Rais Magufuli, yeye kilichombeba ni uwajibikaji wake tangu akiwa Naibu waziri mpaka waziri na sio maigizo unayoyafanya wewe na Kama hutabadilika wewe Urais utausikia redioni tu hautaupata kamwe.

Kumbuka mwaka 1985 kulikuwa na watu maarufu waliyojiandaa kuwa Rais baada ya Baba wa Taifa kusitaafu lkn hawa kupata badala yake Mh, Mwinyi ndo kapata vivyo hivyo mwaka 1995 kulikuwa na mtu maarufu zaidi yako aliyeweza kubadili mpaka jina kutoka jina la kikiristu mpaka uislamu na kapewa maela mengi kutoka Libya lkn jina Lake halikuingia hata 5 bora miongoni mwa wagombea 17 hatimae Mh, Mkapa kaibuka kidedea.

Vivyo hivyo, mwaka 2015 kulikuwa na mtu anaitwa Edward Lowasa aliyejiandaa zaidi ya miaka 20 kuwa Rais, akiwa anatumia njia mbadala hadi za kumuhujumu Mh, Kikwete kwenye teuzi kwa kuwapigia simu waliotakiwa kuteuliwa na kuwambia nimempa Mh, Rais jina lako jiandae atakuteua na baadae wanapoteuliwa wakawa wanamsifu na kumheshimu yeye.

Ushauri wangu Kwenu mawaziri fanyeni kazi kwa bidii acheni kampeni za Urais 2025, hii sio kazi yenu ni kazi ya vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi yetu, pamoja na wananchi wakisema ni wewe utakuwa tu na wasipo kutaka hautakuwa hata kwa dawa.

Kero nyingine, ni kwa wakuu wa mikoa na wilaya ni ukweli usiopingika Mh, Rais alijitahidi kufanya uteuzi makini katika ngazi hizi mbili wengi ni watu makini na hodari katika kazi wasiopenda kujikweza na wanaoipenda CCM kweli na wanajikita zaid ktk utatuzi wa changamoto za wananchi.


Lakini katika msafara wa Mamba na Kenge wamo, hawa Wakuu wa mikoa na wilaya wapo wachache ni waigizaji hawafanyi kazi kabisa!!!! Kuna baadhi ya wakuu wa mikoa wanatumia pesa nyingi kujinadi kwenye TV, Magazeti, Radio na mitandao ya kijamii ili waonekane wanafanya kazi lkn ukweli ni kwamba ni waigizaji kweli nina imani hata Mh, Rais unawajua hawa waigizaji

Kwamfano, Kuna mkuu mmoja wa mkoa alitangaza oparesheni zaidi ya sita kwenye mkoa wake mpaka sasa zote ukimuuliza hakuna iliyotekelezeka hata moja, sasa wananchi na wanachama wa CCM tunajiuliza lengo Lake hasa ni nini? Au anatumia hizi oparesheni Kama kitega uchumi kwake? anatangaza ili watu wajisalimishe kwake na kumpa mlungura? Mimi na wewe hatujui lkn nina imani vyombo vya ulinzi na usalama vina majibu ya haya maswali yote na Kama vina majibu hakika Mh, JPM atayapata pia.


Hawa wakuu wa mikoa na wilaya waliyoajiri vijana wakuwapiga picha kwa kila wanachofanya na kurusha kwenye mitandao ya kijamii hizo pesa wanazowalipa wanatoa wapi? Na wanafanya hivyo ili iweje? Nani anataka kujua leo mkuu wa wilaya au mkoa fulani kafanya hiki Kama sio wananchi husika ktk wilaya husika? Kama sio kutojiamini, uoga na maigizo ni nini!!!!


Kwanini msijifunze kwa Mh, Humphrey Polepole ambae hajawahi kuonekana kwenye media hata siku moja Lakin ukienda Musoma mpaka leo wanamlilia, nenda wilaya ya Ubungo wanasema hakika hawataweza kumpata mkuu mwingine wa wilaya Kama POLEPOLE kwa jinsi alivyo kuwa anafanya kazi yake kwa makini.

Pia jifunzeni kwa mkuu wa mkoa wa Singida aliyepandishwa cheo kuwa katibu mkuu wa wizara na mkuu wa wilaya Mtwara, hawa wote walikuwa hawajipigi picha na kurusha kwenye magroup.


Fuatilieni Wakurugenzi wote wa mashirika ya umma Kama NSSF, TBC, NHC na mengine mengi wanafanya kazi nzuri sana lkn hawahongi vyombo vya Habari ili viwaoneshe au makatibu wakuu wa wizara na Wakurugenzi wote wa Halmashauri za manispaa, majiji na miji wanafanya kazi nzuri kweli.

Jambo lingine baya, ni kitendo cha wakuu wa mikoa na wilaya kuwatukana watumishi wa umma hadharani kumbukeni CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi kwahiyo hata hawa mnaotukana bila kosa ni wana CCM na wapiga kula wetu na waliomchagua Mh JPM zaidi heshimu utu wa kila mtu fanya utafiti kabla ya kumtukana mtumishi wa umma na zaidi fanyeni vikao vya ndani na watumishi wa umma kabla ya kuwatukana hadharani.

Nimeamua kuongelea hili kwasababu juzi kati mkuu mmoja wa mkoa alimtukana hadharani mtumishi wa umma bila sababu za msingi, kulingana na maelezo ya mtumishi yule hakuwa na kosa na Kama mkuu huyo wa mkoa angeanza kufanya vikao vya ndani nae asinge mtusi kiasi kile, kumbukeni kutukana mtumishi wa umma sio umahiri wa uongozi bora na kuonekana kuwa wewe unafanya kazi jifunzeni kwa Mh, Rais na waziri mkuu wake wanapoenda sehemu kabla ya kuhutubia ni lazima afanye kikao cha ndani na watumishi wote baadae ndo anatoa maagizo.

Mh, Rais hata Kama ni ziara ya kushutukiza anapokea kwanza maelezo ya taasisi husika halafu ndo anachukua hatua, sasa ninyi baadhi ya wasaidizi wake sijui mnaiga kutoka wapi.

Mfano, unamkuta mkuu wa wilaya au mkoa anamtukana mwalimu hadharani tena mbele ya wanafunzi, bila kujua kuwa mwalimu ni mtu anayeweza kupunguza au kuongeza kura za ccm kwasababu yeye anafundisha watoto wetu na wadogo zetu na wanafunzi humsikiliza sana mwalimu kuliko mtu yeyote kwahiyo kitendo kile kinaweza kusababisha wao wapandikize chuki miongoni mwa wanafunzi.

Pia, kwakufanya hivyo kunaweza kusababisha wanafunzi wasimheshimu tena mwalimu wao na wasipo mheshimu maana yake hawatazingatia anachowafundisha mwisho wake watafeli mitihani.

Kwa wale, wateule wa Mh, Rais serikalini na ndani ya chama naombeni mridhike na madaraka mliyopewa kwani haya yote mnayafanya kwasababu ya uroho wa madaraka, unamkuta mtu ni mkuu wa mkoa bado anafanya juu chini awe katibu mkuu wa CCM Taifa, mtu ni waziri anajitahidi ili awe Rais wa nchi na Mwingine ni waziri anataka awe makamu mwenyekiti wa CCM Bara. Tambueni chama cha Mapinduzi kina watu zaidi ya milioni 8na wengi wasomi je wao wataongoza lini? Fanyeni kazi vyeo vipo mpaka mbinguni mtapata tu.

Mwisho naombeni wote niliyowagusa mjisahihishe maana huu ndo ukweli na ukiona mimi mmoja nimejitoa mhanga nakuandika ujue wako wengi mnawakela ila wanaogopa kusema kwakuhofia kukosa uteuzi, kuharibu kazi au kutishiwa

Mimi binafsi siogopi kutishiwa kwa namna moja au nyingine japo najua wengi mtanitafuta inbox, kumbukeni anayenitishia mimi anamtishia Mungu maana mimi nimeumbwa kwa Mfano wa Mungu.
Kwa wale waoga wote wataogopa kukomenti na ku like makala hii.
Imeandaliwa na,
Comrade
Mwita nyarukururu
Mpinga mafisadi
 
Kwenye bandiko lako kuna sehemu sizjaielewa vema Labda waja watatusaidia na kutupa ushahidi wa hayo matukio. Hebu tupeni ukweli wa hii aya. Hivi Polepole analiliwa Musoma na Ubongo? Hivi hiki kitu kimeshawahi kutokea?
Umeandika "Kwanini msijifunze kwa Mh, Humphrey Polepole ambae hajawahi kuonekana kwenye media hata siku moja Lakin ukienda Musoma mpaka leo wanamlilia, nenda wilaya ya Ubungo wanasema hakika hawataweza kumpata mkuu mwingine wa wilaya Kama POLEPOLE kwa jinsi alivyo kuwa anafanya kazi yake kwa makini."
 
Hujaitendea haki dhima ya jamii forum

"Where we dare to talk openly"
 
Kwenye bandiko lako kuna sehemu sizjaielewa vema Labda waja watatusaidia na kutupa ushahidi wa hayo matukio. Hebu tupeni ukweli wa hii aya. Hivi Polepole analiliwa Musoma na Ubongo? Hivi hiki kitu kimeshawahi kutokea?
Umeandika "Kwanini msijifunze kwa Mh, Humphrey Polepole ambae hajawahi kuonekana kwenye media hata siku moja Lakin ukienda Musoma mpaka leo wanamlilia, nenda wilaya ya Ubungo wanasema hakika hawataweza kumpata mkuu mwingine wa wilaya Kama POLEPOLE kwa jinsi alivyo kuwa anafanya kazi yake kwa makini."
Hata kukosoa ni jambo la msingi endeleeni
 
Ungeweka na namba ya simu ili tukikufikiria nafasi basi tukupate kwa urahisi
 
Hata kukosoa ni jambo la msingi endeleeni
Kwa ufupi ni kwamba, nilitaka kupata ushahidi wa matukio ya kilio cha wananchi kwa huyo bwana na wala sio maneno matupu. Kama unayo ni vema ukatuonyesha ili tuudhihirishie umma kwamba jamaa alikuwa ni mchapakazi.
 
Huu upuuzi haukufaa kuwekwa hapa, ulitakuwa kupelekwa kule kwenye majukwaa ya majungu kama CCM ushindi & the like. Si ni nyie ndo mlimweka ndani Maxence Melo? Lingefungwa hili jukwaa huu umbeya wenu mngeupitishia wapi?
 
Ajabu huyo Polepole unayemsifia amepata kadi ya ccm baada ya kupata ukatibu uenezi. Hakuwa mwanachama wa ccm kabla yake, alikuwa mwanaharakati tu. Kadhalika mwenye kadi ya uwanachama wa mkuu zaidi inayoonyesha uanachama wake tangu enzi za Nyerere atupe kopi hapa.

Kwa ufupi chama kimevamiwa na wanachama halisi wameamua kukaa kimya. Hao wasaidizi unaosema wako kimya jaribu kuwatafuta kwa wakati wako binafsi wakuambie yaliyopo mioyoni mwao. Utashangaa na kujuwa kwamba laana tuliyonayo sio ndogo. Hao mawaziri usidhani wanafuraha kuitumikia nchi, hawana. Kama sio mkate wao na ugumu wa fursa nyingine nakuhakikishia wengi wangeomba kuachia ngazi.

Hawastahili kulaumiwa, waliotufikisha hapa na wanaotubakisha hapa ndio wanaostahili kulaumiwa. Hata wewe ungepewa uwaziri yawezekana tusingekusikia. Tuliombee tu taifa letu huku tukiangalia mishale ya saa na kalenda.
 
Ptuuuuu...hakuna ulichoandika hapo...umeanza kujinadi kwamba utaandika vitu dhahiri kabisa mwisho wa siku umetuandikia vitendawili...
 
Back
Top Bottom