Ushauri: Mpenzi wangu ataniua!

Mangole Valles Michael

JF-Expert Member
May 30, 2021
333
671
Siku za nyuma niliandika kisa cha mapenzi na safari yangu ya kuanza maisha upya ndani ya mkoa mpya.

Update: nilipo fika mkoa X mambo yangu kwakweli hayajaenda vizuri kama ilivyo kua matarajio yangu lakini napambana kwakua najua nilikotoka nimemuacha mpenzi wangu anaishi kwangu gettoni.

Siku ya leo kanitumia sms ya Salam baada ya Salam kwa njia ya sms nikamuuliza unafanya nini, akajibu bado kalala nikamuuliza kwanini umelala mpaka saa hizi saa 4:30 akajibu mvua inanyesha na hana cha kufanya.

Binafsi nikajibu sawa, baada ya hapo akasema nataman kusafari kwakuwa najihisi mpweke lakini sina sehem ya kwenda, nikamwambia hata kipindi naondoka nilitaka usafiri kwakuwa nilijua Mambo haya yatatokea ungesafiru wakati huo ili kupunguza hali ya upweke. Na nikweli nilimwambiaga kuwa asafiri,

Baada ya hapo kabla hajajibu sms yangu nikamtumia sms nyingine ikisema, baadae nikipata nafasi nzuri nitakupigia simu nikuelezee hatua gani nimefikia huku niliko, changamoto Zinazonikabili, lakini pia tutajadili namna ya kufanya tuone tunafanyaje, nia ya sms yangu ilikua ni kuchambua hali yangu ya uchumi kwakua dem huyu nimekaa nae miaka 3 sasa kwaio sina cha kumficha ananijua vizuri, ajabu ikaja kwenye sms yake ndo iliyo nifanya niandike hii thread ameandika hivi.

"Haina Haja Ya Knambia Ha2a Ulofikia Me Nimesha Jua Tiyal Me Kuku Uliza Nataman Kusafil Ulivo Nijib2 Nikajua Kabsa Ww Huko Uliko Haujawa Tiyal Kulud Huku Wala Mm Kuja Kwahy Haina Haja Ntajuwa Mimi Jins Yakuish Wala Usjal Pambana2 Wala Me Stakuuliza Tena Saw"

Dah! Kweli mpaka saiv sjamjibu namfikilia sjui nimjibu nini huyu mtu.
 
Huyu ndo yule mwanamke aliye kua hataki kukuruhusu kwenda mkoa mwingine?

Kama ndiye basi jua hukua na baraka zake katika hiyo safari na ndio maana wenda mambo hayajaenda sawa.

Kuhusu text yake mkuu, tuliza kichwa mpigie simu mueleze yote ya muhimu anayofaa kuyajua na jiandae kwa both action reaction kutoka kwake.
 
Ndivyo wanawake tulivyo. Lile swali lake lilikua linauliza kinyume. Alimaanisha natamani nisafiri nije huko ila ndo akaandika vile akitegemea utamwambia njoo huku mpnz ila ulivyojibu vile tayari kichwa chake kimebeba picha nyingine. Kweli mlipoambiwa muishi na sisi kwa akili, including these shits. We are not always straight
 
Mimi nilidhani ni huyu tu bibie ndo uelewa wake mdogo kumbe ni nature yanu wanawake? Dah sasa unanishaurije Nimfanyeje ili kidogo akae sawa?
 
Huh!! Sasa hapo hujaelewa nini? Au mgeni wa wanawake?
 
Ndivyo wanawake tulivyo. Lile swali lake lilikua linauliza kinyume. Alimaanisha natamani nisafiri nije huko ila ndo akaandika vile akitegemea utamwambia njoo huku mpnz ila ulivyojibu vile tayari kichwa chake kimebeba picha nyingine. Kweli mlipoambiwa muishi na sisi kwa akili, including these shits. We are not always straight
Ashukuru umemsaidia kweli hapa. Sijui kapotelea wapi. Come back dude and get this for you!!
 
Ndivyo wanawake tulivyo. Lile swali lake lilikua linauliza kinyume. Alimaanisha natamani nisafiri nije huko ila ndo akaandika vile akitegemea utamwambia njoo huku mpnz ila ulivyojibu vile tayari kichwa chake kimebeba picha nyingine. Kweli mlipoambiwa muishi na sisi kwa akili, including these shits. We are not always straight

mimi huo ujinga ndio huwa siuelewi, yaani unataka D, lakini unanzia A , B ukitegemea mimi nijue kuwa unataka D?
 
Back
Top Bottom