Ushauri: Mpenzi ana hasira na kununa, nifanyaje?

Ushauri: Mpenzi ana hasira na kununa, nifanyaje?

karim02

Member
Joined
Apr 25, 2016
Posts
64
Reaction score
40
Poleni na majukumu wakuu,

Samahani kwa thread ndefu, lakini lengo ni unielewe.

Kwa kifupi, kuna msichana ambaye ninaishi naye, namaanisha tumepanga nyumba moja, ingawa yeye ndio alotangulia kuhamia hapo. Mbali na hayo msichana huyu alinivutia sana, nikamwomba urafiki wa mapenzi akakubali na tukaingia katika uhusiano.

Tazizo la binti huyu ni hasira, hususani anapofikiria jambo flani kuhusu mtu flani au kitu flani huamini kuwa ni kweli, bila kufanyia uchungunzi wa jambo husika na kama fikra zake zitamuumiza atanuna na anaweza asikusemeshe kwa muda wa siku kadhaa. Hili lilikuwa changamoto kubwa kwangu, nilijaribu kuzungumza nae mara nyingi kuhusu tatizo lake hilo sijui kama alikuwa ananielewa au ni jeuri tu, hakubadilika.

Maisha yaliendelea, siku moja alinishutumu kuwa nina uhusiano na msichana mwingine na akaniambia hawezi kuwa nami tena sababu hapendi kuumizwa, nilimuuliza kama ana ushahidi wa hilo bali hakuwa na jibu zaidi ya kusema kuwa anasikia tu kwa watu. Nilimweleza tabia za walimwengu walivyo na nikamwambia ni jinsi gani watu wanavyoweza kuleta husda kwa wapendanao, bali hakunielewa na akadai tuachane.

Nilijisikia vibaya sana nikamwomba asichukue uamuzi ule bali afanye uchunguzi, ila hakunielewa na msimamo wake ulikuwa ni ule ule kuwa tuachane. Daah! Kiukweli iliniuma na sikuamini, nikaona bora nimwombe radhi ili yaishe tuendelee na penzi letu. Alikataa na kusema uamuzi aliochukua ni sahihi na hakupenda nimsumbue.

Mapenzi yanauma ukizingatia nilimpenda sana, sikuishia hapo niliwaeleza marafiki zake wa karibu kuhusu tofauti zetu, nao walimweka chini wakamwelewesha kuhusu changamoto zilivyo katika mapenzi ila hakuwaelewa na jibu lake lilikuwa ni lile lile kuwa hanitaki tena. Niliumia sana nikajuta kwanini niliingia katika mapenzi na binti yule.

Hata hivyo kama mjuavyo moyo ukishapenda ni shida, nilitafuta njia mbalimbali za kumsogeza karibu yangu tena ikiwemo kumpigia simu mara kwa mara na kumpa zawadi tofauti, lakini cha kushangaza aliniblack list na akaniblock whatsap, yani nilijiuliza ni kweli kosa lile ndo limepelekea kunichukia kiasi kile au alikuwa na sababu zingine? Sikupata jibu, nikaamua kutulia ingawa moyo ulikuwa ukiniuma sana hususani nilipokuwa namuona ndo kabisa.

Siku zilisonga mbele taratibu nikaanza kumsahau, tukawa tunapishana na kusalimiana kama watu wengine au kama kaka na dada. Baada ya muda mwingi kupita nilipata mpenzi mwingine na sababu sina kipingamizi chochote, siku moja nilimkaribisha nyumbani huyo mpenzi wangu mpya. Mpenzi wangu wa zamani hata nikimsalimia hataki kujibu, nimekuwa nikijiuliza kwanini ananuna?

Nambie mkuu wewe unadhani ni kwanini na nifanye nini kuhusu hilo?
 
Kununa ni kawaida sana. Ni ngumu kwa baadhi yetu kuona mwenzio amemove on na maisha yake. Kama unaleta hapo mtu bora uhame...
 
Hama nyumba iyo na hata huyo mwanamke wako mpya akijua hiyo atajua unamu expose kwenye risky ya kupata shida.
Unadhaani kuhama nyumba ni suluhisho? huoni kuwa hata nikihama bado anaweza kuleta fitna na ugomvi huko niliko mkuu?
 
mkuu tayari ushafanya maamuzi. Kurudi nyuma ni sawa na kulamba matapishi. Km alishindwa kukusamehe na sasa una mtu wako sio vizuri kurudi nyuma.
Mpaka kufika hatua ya kuomba humu ushauri inaonesha kwa jinsi gani unavyompeda kuwa na msimamo kama mwanaume.
Huyo wivu unamsumbua tu
 
Hakuna kurudi nyuma wala kuhama nyumba. Kwa kuwa ni yeye aliyeamua kusitisha uhusiano kwa sababu amvazo hakuwa na uhakika nazo, basis ni vema ajifunze kutokana na makosa yske mwenyewe. Naamini akimpata mwingine atakuwa makini.
 
Ana wivu wa kizamani!We endelea na maisha tu ulifanya jitihada za kutosha, cha muhimu mweleze demu wako mpya ili asijekuzulia sokomoko
 
da
Ana wivu wa kizamani!We endelea na maisha tu ulifanya jitihada za kutosha, cha muhimu mweleze demu wako mpya ili asijekuzulia sokomoko
daaah ni kweli mkuu ila nipo ktk wkt mgum sana .
 
Back
Top Bottom