Wazo zuri maana huyo mzee alijiepusha na siasa za majitaka, hivyo watu wengi wako naye.
Wazo jema, Mkuu. Ngoja tusubiri wahusika watalichukuliaje...Kutokana na hali halisi na kwa kuzingatia Mengi amegusa watu wengi ktk nchi hii, basi watu wengi wangependa kumuaga kwa makundi tofauti.
Kwa maono yangu Karimjee hapatoshi kuhimili idadi ya watu wataopenda kutoa heshima za mwisho, karimjee kuna hali ya kaubaguzi wa aina ya watu kuingia hivyo kufanya watu wachache waweze kumuaga.
Kwa muktadha huo kamati inayojihusisha na mazishi yake ipeleke mwili uwanja wa taifa ili kila mtu aweze kuaga.
Anataka kuufanya msiba wa chama?Bashite ni sawa na mbwa mwitu hachagui hata mzoga wa mbwa mwenzie hula.