Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 16,003
Igwe wana JF!
Nimelazimika nimshaurriMbowe na WWabunge wake kurejea bungeni iijapokuwa kuna aibu mtakayopata kutokana na kiapo chenu ambacho hakina mantiki.Zingatia yafuatayo;
Wananchi katika majimbo takriban 70+ ya UKAWA wamekosa mtu wa kuhoji utekelezaji wa miradi ya barabara,afya,elimu nk na jana alhamisi KUB Mbowe umekosa fursa ya kumuhoji waziri mkuu maswali ya papo kwa papo.Mmetutia hasara!
Sababu zenu za kugoma ni malalamiko tu ambayo huwezi kumtia mtu hatiani,chuki yenu kwa Naibu Spika ilianza tokea siku ameteuliwa na CCM,mlitoa vijisababu vingi na hata kupendekeza baadhi ya wabunge ndani ya CCM angali mlikuwa na mgombea wenu Magdalena Sakaya.Mlitengeneza chuki binafsi na hata Lissu akahoji ni lini Tulia alijiunga CCM?,ni moja ya swali la kisiasa ambalo kimantiki na kiueledi huulizwa na mjinga.
Kwasasa mmeshotoa hati kwa Spika ya kumvua madaraka Naibu Spika sasa ili kuheshimu demokrasia yawapasa muingie bungeni mkisubiri hatma.Kule Afrika kusini mara kadhaa wabunge wa upinzani wametoa hoja kumuondoa spika wa bunge Bi.Beleka Mbete na wameshindwa kwa hoja na kura bungeni bila kutoka.Msiporudi Bungeni na hoja yenu ikashindwa dhamira zenu zitawasuta na mtajikuta mkitekeleza majukumu kwa kiwango cha chini.
Mmeonyesha silaha zenu za mwisho ndani ya miezi sita hakika mmejiweka katika nafasi kubwa ya anguko.Serikali imefanya mambo muhimu mapema ambayo kisiasa ni lazima uyafanye sasa ili katika mwaka wa tatu,nne na tano wa awamu ya kwanza wananchi wapate matunda ya mabadiliko hivyo kujihalalishia ushawishi kwa wananchi wengi walio maskini.Awamu ya kwanza ya mkapa alibezwa sana mwanzoni,watu wakaita zama za ukapa/ukata kutokana na sera ya kusimamia misingi na kubana matumizi na wananchi wakamwamini wakamchagua tena 2000 kwa asilimia 82 kutoka 60 aliyopata 1995.
Wanafunzi wa Chuo kikuu waligoma kudai nyongeza ya "boom" kutoka 1500 hadi 2500,Mkapa alimtuma aliyekuwa Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Bw.Ahmed Mbegu kuzungumza na wanafunzi, wakakataa eti wanamtaka Raisi manake Sumaye alidharaulika sana na jumuiya ya Chuo kikuu,mgomo ukazidi likabandikwa tangazo kuwa kufika saa 10 jioni hairuhusiwi mwanafunzi yeyote kuonekana hostel wala darasani FFU wakasimamia zoezi kwa virungu na vichapo kwa waliokaidi.Baada ya hapo migomo ya kijinga iliisha na kubaki masuala ya msingi.
Mbowe na wabunge wengine wa Ukawa hamna jinsi aibu ya kiapo haiepukiki japo ni busara kurudi mapema kwa sababu hamtapata matokeo na watu wameshawaona nyie ni wakawaida.
Nawasilisha.