Kama, unazungumzia kuajiriwa umepotea bora tu hiyo hela ya kusomea hizo program ukalime mashamba au fanya biashara ili baadaye usije leta mrejesho baada ya miezi 18 au 24ya masters yako ukaanza kulialia.
Sikukatishi tamaa, ila wazo la kuajiriwa unapoenda kusoma litoe kwanza katika mipango yako.
Zaidi, twambie ni kwa nini unaenda kusoma hiyo masters maana hujamaliza hata academic year moja tangia umehitimu hiyo bachelor yako.
Mwisho, program yoyote inasoko pale tu utakapo jitambua wewe binafsi kuwa unahitaji kuwa wapi na kufanya kazi ipi.
Ila kusema.kuhusu soko la ajira kwa kufatisha program aliyosoma mtu hiyo bado sana.