Wanabodi,
Huu ni ushauri wangu wa bure kwa Mhe. Edward Ngoyai Lowassa kuwa japo amerejea nchini akiwa fit na yuko tayari kwa mapambano yoyote, namshauri asitumbukize mguu wake kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa Arumeru ili asimponze bure Sioi!.
Mimi ni miongoni wa wale wakweli wachache humu jujwaani "we take people for who they are not what they are" hivyo tunamkubali Lowassa kwa uwezo wake wa maneno machache na vitendo virefu, tofauti na wenzetu wengi humu wanaowashangilia watu wa maneno mareefu na vitendo sifuri!.
Nimemshauri Mhe. Lowassa asitie mguu Arumeru kwa sababu Sioi anaweza kusimama mwenyewe na kutembea bila "walker"!, na pia anaweza kukamata kijiko na kula mwenyewe bila kuhitaji kulishwa, "spoon fed" na ba mkwe!.
Kufuatia maneno maneno ya the role of EL kwenye uchaguzi wa ndani wa CCM kulikopelekea Sioi kupitishwa, let this role end off inside CCM sasa "its high time let the people say!" tusiwasemee wana Arumeru kwa fulana, kofia na shibe ya siku moja!, Tuwaache wana Arumeru wajichagulie chaguo lao ambalo tayari walishachagua wanasubiri tuu kuthibitisha, hivyo Lowassa hana sababu kabisa hata ya kutumbukiza mguu wake ili kijana athibitishe amepata ushindi wa kishindo wa yeye kama Sioi na sio kushinda kwa kusaidiwa na ba mkwe!.
Ingekuwa Sioi ni mwana CCM mwingine tuu wa kawaida asiye na nasaba yoyote na Lowassa, ningemshauri Lowassa apige kabisa kambi Arumeru, lakini kwa vile Sioi na yeye ni mtu na mkwewe, Lowassa akitia mguu Arumeru na atatibua ushindi laini wa Sioi kuonekana umepatikana kwa nguvu za ziada ambazo kiukweli hazihitajiki!.
Juzi nilifurahi kumuona EL ITV kwani sasa wamelift ile ban yao kwake, na aliposema yuko fit kwa mapambano yoyote, namshauri ahifadhi nguvu zake kutengeneza the "winning coalition" yake ndani ya uchaguzi wa ndani wa CCM ili 2015 yeye ndie apitishwe kuwa mgombea wa CCM huo ufit wake aje auonyeshe kwenye uwanja rasmi wa mapambano ya kweli ili tupate rais kutoka Kaskazini na kupata ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania!.
Naomba kuawasilisha.
Pasco
Update
Wanabodi, kushindwa kwa Sioi ni matokeo ya kuupuuza ushauri huu!.
Mimi nilimtegemea Sioi ashinde kwa kura za symphathetic votes ili kumfuta machozi ya kufiwa. EL kamponza kijana kapigwa chini!.
Wenye uwezo wa kunielewa naomba mnielewe, wale wengine msio na uwezo, nieleweni hivyo hivyo mnavyoelewa maana huo ndio uelewa wenu.
Pasco.