sonaderm
JF-Expert Member
- Nov 9, 2015
- 618
- 1,816
Habari wadau!
Siku kadhaa zilizopita nilimsikiliza bwana Ruge akizielezea fursa 10 za biashara au ujariamali hapa nchini..Kwa kuwa waliweka promo nyingi sana juu ya hicho kipindi maalum nikaona nimsikilize lakini nilichogundua hakukuwa na jipya kwenye hizo "fursa" na kwa upande wangu naona ametuelezea ''ideas" za biashara..
Tatizo kubwa linalowasumbua wengi hasa wajasiriamali na wafanyabiashara ni issue ya mitaji na namna ya kuisimamia biashara ili iweze kuwa sustainable na kukuwa.Na hilo ndio eneo ambalo bwana Ruge alipaswa kujikita nalo kama sehemu ya kuwasaidia vijana!
Bila shaka hata humu jamii forums zimeshajadiliwa hizo ideas. Ki ukweli Ideas ziko nyingi kama alivyozitaja lakini kama hakuna mitaji na watu hawana elimu ya usimamizi wa biashara basi hakuna shaka hawawezi kufika popote.Kwa nguvu kubwa iliyotumika kutangaza kipindi basi ni mategemeo yangi next time ajikite zaidi kuelezea namna za kupata au kukuza mitaji na usimamizi!Kwa upande wangu ndio naona changamoto katika ujasiriamali ambazo inabidi ziwe ndio ''issues to discuss'' ili ziwasaidie vijana.
Mabenki kwa sasa hayashikiki kwa riba na hata watu wakikopa bado watu hawana ujuzi au elimu ya kusimamia hiyo mikopo kwenye biashara zao na mwisho wa siku huishia kwenye majanga!
Mbali na hilo, wakati anazisema hizo ''fursa'' hakuweza kuelezea kwa kiasi gani mtu anaweza kujiingiza na kupata faida kwenye hayo maeneo aliyoyataja, ,maelezo yake yalikuwa mepesi sana ni kama mtu yupo kijiweni anakwambia kumiliki boda boda kunalipa bila kudadavua kunalipa kwa namna gani!
Kama muda wa kipindi ulimbana na alishindwa kuelezea into details basi ingekuwa busara angezipa session na kuelezea chache kila siku lakini kwa undani wake ili mtu mwenye maamuzi ya kufanya hicho kitu awe kweli amepata information za kutosha kuliko maelezo ya juu juu!
Mwisho kabisa, mitaji na elimu ya usimamizi wa biashara ndio eneo linalopaswa kuwa kipaumbele katika kuwawezesha vijana wa kitanzania..