Ushauri kwa Wizara ya Elimu

Ushauri kwa Wizara ya Elimu

Joined
Jul 29, 2016
Posts
38
Reaction score
67
6:4:2:3+ UFANYIWE MAREKEBISHO HAYA YA MSINGI KUNUSURU ELIMU YETU.

NA ALLY RAMA.

Naandika maoni Haya nikiwa na imani kubwa kuwa itawafikia walengwa na maoni yangu yatachukuliwa kwa uzito Mkubwa..

Kuna jambo kubwa sana linaendelea kwenye mfumo wetu Wa elimu linalohusu mabadiliko ya mtaala Wa elimu ya msingi/na ile ya upili..

Mabadiliko Haya yana nia njema kabisa ya kufanya elimu ya kidato cha NNE kuwa elimu haki ya msingi na elimu ya msingi ambayo Kila mtanzania Mwenye umri Wa miaka 7 aipate..

Hii maana yake ni kuwa; Sasa hivi ukianza darasa la kwanza; utaishia kidato cha NNE moja kwa moja..

Ni tofauti na zamani ambapo elimu ya msingi iliishia darasa la saba...

Maandalizi ya kuupokea mfumo huu mpya yameanza km ilivyoelezwa kwenye Sera mpya ya elimu ya mwaka 2014..

Moja ya maandalizi hayo ni kuandaa walimu ambao Sasa hivi; walimu Wa daraja la IIIA hawadahiriwi tena kwenye vyuo Vya ualimu na badala yake; wanadahili diploma ya elimu ya msingi kwa miaka mitatu..(diploma in primary education)..

Hata viwango Vya ufaulu Ili kuweza kujiunga na diploma hii vimeongezwa toka div 4 point 28 hadi division 3 mwaka huu..

Haya ni mabadiliko chanya kwenye elimu yetu na ni ya kuungwa mkono..

Jambo kubwa lingine ni muda Wa elimu ya msingi..

Miaka 10 badala ya saba/11..
Nitafafanua..

Zamani elimu ya msingi iliishia darasa la saba..
Sekondari hadi kidato cha NNE ilikuwa miaka NNE..
Hivyo Ili kumaliza kidato cha NNE; ulihitaji kutumia miaka 11..

Ukiunganisha kidato cha Sita miaka miwili; na kisha chuo kikuu miaka mitatu na kuendelea (inategemea na kozi unayoifanya)..

Mfumo ulikuwa 7:4:2:3+ (ukiondoa elimu ya awali)..

Mfumo Wa Sasa umebadilika; elimu ya msingi ni hadi kidato cha NNE ila Sasa shule ya msingi ambayo ipo ndani ya sekondari itaishia miaka 6 tu..
Kwa hiyo; Ili kumaliza kidato cha NNE unahitaji miaka 10 badala ya 11 ya zamani..

Kidato cha Sita hadi chuo kikuu hakuna mabadiliko..

Mfumo mpya ni huu:
6:4:2:3+ badala ya ule Wa zamani Wa 7:4:2:3+

kwenye mfumo mpya;; hakutakuwa na mitihani ya mchujo kati ya darasa na darasa (darasa la pili unapita free;; darasa la nne free; la sita free; kidato cha pili free)..

Mchujo utaukuta kidato cha NNE..!!!..

kipengele cha lugha ya kujifunzia na kujifundishia ni kiswahili kwa shule ya msingi (ambayo Sasa itaishia kidato cha NNE) na baadae kiingereza kwa kidato cha sita hadi chuo..

Yaani utasoma English km somo ila utafundishwa kwa kiswahili masomo yote hadi kidato cha NNE..

Ukifika kidato cha tano unabadili lugha ghafla na kuanza kiingereza..(full ung'eng'e)


MAPENDEKEZO YANGU..

1: Kuhusu lugha ya kijifunzia; napendekeza tutumie kiingereza toka elimu ya msingi hadi chuo kikuu..
Sioendekezi kabisa kiswahili kitumike hatua yeyote ile kwenye elimu yetu..
Wala tusijifunike kwenye tanuri hewa la uzalendo kwenye hili..

Nitaandaa andiko mahsusi kwenye hili..
Hili la kumfanya Mtoto aanze kusoma kwa kiingereza kuanzia kidato cha tano haikubaliki na ni juhudi za kuwafanya watoto wakariri na Sio kuelewa..

Na usipoelewa hujifunzi..
Na usipojifunza huwezi kuwa mtaalamu (practitioner)..

Usipowapata wataalamu utatengeneza taifa la watu Wa mwendokasi..

2: kuhusu mfumo Wa 6:4:2:3+; napendekeza tuwe na ule Wa 8:4:3+..

Pendekezo hili linalenga kuondoa kidato cha tano na Sita kwenye mfumo wetu Wa elimu bila kuathiri content zake..

Yaani; syllabus ya kidato cha tano na Sita tuziingize o-level..

Cha kufanya..
Kwanza elimu ya msingi ya zamani iishie darasa la nane ambapo syllabus ya form one na two itakuwa ndani yake..

Ukifika form one utaanza kusoma sylabus ya kidato cha tatu kuendelea hadi Sita..

Na hii si dhana mpya..
Hadi Sasa hivi; reproduction ya kidato cha tatu inasomwa darasa la Sita ila kwa kiswahili..

Kenya wanatumia mfumo huu pia..

Ni mfumo Rahisi sana km tutakuwa tunatumia lugha moja ya kujifinzia na kufundishia..

Kwa maoni yangu; kidato cha tano na Sita ni wastage of time..
Ni elimu inayoua malengo ya wengi hasa masomo ya sayansi..

Heri tungeweka diploma km elimu ya lazima kuliko kidato cha Sita..


Jambo lingine kubwa ni kuingiza mitihani ya mchujo kati ya darasa na darasa..

Huwexi kupata elimu bora na watu bora bila kuwapima na kuwachuja..

Hii pitisha pitisha tu bila mchujo imetugharimu sana kwa siku nyingi..


Na kwa wasiofaham; private schools zinafanya vizuri kwa sababu ya screening..

Tuwachuje watoto wetu..
Vipanga Twende nao na vilaza (in magufuli's voice) tuwaondoe..

Elimu ya mwendokasi haikubaliki..

Tusemezane.
 
Back
Top Bottom