Ushauri Kwa Watafuta Ajira.

Ushauri Kwa Watafuta Ajira.

Troll JF

Platinum Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
9,306
Reaction score
13,743
Sasa hivi Tumefikia katika kipindi ambacho kuna Graduates wengi sana katika Kila Kada hadi Urubani ambao Una Ada Kubwa Sana.

Nizungumzie Masuala Ambayo yanaweza Kukosesha Marks hasa Kwenye Oral.

Suala La Kufuga Ndevu
Siku hizi Kuna Vijana Wengi Sana Wanafuga Madevu wakifuta tamaduni za Nje Kwa Kuwaangalia Akina Rick Ross au Wengine Katika Mihangaiko yangu ya Kutafuta Kazi Sijawahi Kukutana hata Msaili mwenye Ndevu Iweje msailiwa Ufuge Ndevu Tubadilike Tujitahidi Kuondoa Ndevu Ni dalili ya Usafi. Kuzichonga Ndevu mnaita O kama wanavyofanya wasanii si Busara pia.

Kunyoa Denge/Pank/Kiduku

Graduate ambaye unategemewa Kukabidhiwa Majukumu ndani ya Ofisi za Serikali Unanyoa Kiduku tena wakati wa Usaili Si Sahihi nashauri muwe mnanyoa Low -Cut au Kipara kwa Mtu aliyeanza Kutoka Upara mapema.

Mavazi
Ni aibu kwa Kijana Unamkuta kavaa Kisuruari Kimembana hadi anashindwa Kutembea wengine wanavaa Jinsi la Suruali hili ni tatizo la Akina Dada wenye Makalio Makubwa Wanapenda sana Kuvaa Suaruali ili Kuyaonesha Hivi vitu vinaweza ku discredit Taaluma yako.

Suruali ya kitambaa na Shati hasa za Rangi moja Mi ndo huwa naona the Best.

Viatu
Kutokea na Raba Si Ustaarabu wengine nao Huwa wanaenda na Sendols kwa wanaume si Busara. Pia Niliona Dada Mmoja Amevaa Viatu Virefu (High heels) kile Kisigino Kina Urefu kama wa Futi moja Huwezi amini kama Kakivaa Mwenyewe unaweza Kusema Kapandishwa Hapo Be simple na Viatu visivyo na mbwembwe kama A secondary School Girl
 
Safi sana.
Nashauri vyuo vyote vya chini,kati na vinavyotoa elimu ya juu viwafundishe vijana jinsi ya kuandika C.V na barua nzuri za kikazi.
Wanachokionyesha vijana watafuta kazi kwenye mabarua ni aibu, juzi kuna kijana mpaka nikataka kumtandika konde, maana kila ukimwelekeza kakosea afanye marekebisho anabishana nasi. Alipoondoka tukaichukua barua yake tukaichana huku mwenyewe anasubiria kuitwa kwenye usaili.
Umetumia salio lako kumwita aje afanye marekebisho anakuja analeta ujuaji.
 
barua haiitaji mbwembwe mlizo taka nyie, kwani mnataka muajiri kuwa mchapaj hapo ama mkufunzi wa cv.
 
Suala la kufuga ndevu hapo tunatofautina kidogo coz mm ninachojua ni ziwe safi na smart mbona office za serikali na private kuna watu kibao wana ndevu
 
barua haiitaji mbwembwe mlizo taka nyie, kwani mnataka muajiri kuwa mchapaj hapo ama mkufunzi wa cv.
Ndugu yangu kwa tuliopata kazi kwa kufuata mchakato wa sekreterieti ya ajira tunajua kuwa siku hizi hupaswi kuwa lelemama katika kufight ajira wewe kama umeajiriwa kwa ajira za mafungu kama za walimu na watu wa afya au kilimo ni heri utulie tu.
Ukikosea hupati kazi.
Hivi kwenye tangazo mmeshasema kuwa barua zote zipitie kwa meneja kwa anuani hii mtu anaandika barua kwa anuani tajwa ila anamtumia afisa manunuzi eti kisa yeye anaomba nafasi ya Afisa manunuzi msaidizi.
Ukimwambia aiandike upya anamind na vireasons vyake.
Tena si kosa hilo tu niliona makosa mengi ya kiuandishi ikiwemo kuweka sahii mahali palipopaswa kukaa jina na mahali pa kuweka sahihi yeye kuweka jina., Kujitambulisha yeye kama afisa
kwakuwa tu kasomea kitu fulani hata kabla ya kupata kazi.
 
Sasa hivi Tumefikia katika kipindi ambacho kuna Graduates wengi sana katika Kila Kada hadi Urubani ambao Una Ada Kubwa Sana.

Nizungumzie Masuala Ambayo yanaweza Kukosesha Marks hasa Kwenye Oral.

Suala La Kufuga Ndevu
Siku hizi Kuna Vijana Wengi Sana Wanafuga Madevu wakifuta tamaduni za Nje Kwa Kuwaangalia Akina Rick Ross au Wengine Katika Mihangaiko yangu ya Kutafuta Kazi Sijawahi Kukutana hata Msaili mwenye Ndevu Iweje msailiwa Ufuge Ndevu Tubadilike Tujitahidi Kuondoa Ndevu Ni dalili ya Usafi. Kuzichonga Ndevu mnaita O kama wanavyofanya wasanii si Busara pia.

Kunyoa Denge/Pank/Kiduku

Graduate ambaye unategemewa Kukabidhiwa Majukumu ndani ya Ofisi za Serikali Unanyoa Kiduku tena wakati wa Usaili Si Sahihi nashauri muwe mnanyoa Low -Cut au Kipara kwa Mtu aliyeanza Kutoka Upara mapema.

Mavazi
Ni aibu kwa Kijana Unamkuta kavaa Kisuruari Kimembana hadi anashindwa Kutembea wengine wanavaa Jinsi la Suruali hili ni tatizo la Akina Dada wenye Makalio Makubwa Wanapenda sana Kuvaa Suaruali ili Kuyaonesha Hivi vitu vinaweza ku discredit Taaluma yako.

Suruali ya kitambaa na Shati hasa za Rangi moja Mi ndo huwa naona the Best.

Viatu
Kutokea na Raba Si Ustaarabu wengine nao Huwa wanaenda na Sendols kwa wanaume si Busara. Pia Niliona Dada Mmoja Amevaa Viatu Virefu (High heels) kile Kisigino Kina Urefu kama wa Futi moja Huwezi amini kama Kakivaa Mwenyewe unaweza Kusema Kapandishwa Hapo Be simple na Viatu visivyo na mbwembwe kama A secondary School Girl
hoja zakike kabisa yaan we unatutisha tusifuge ndevu unaakili wewe.nisawa nakuzuia bleeed ya mwanamke acha upumbavu wewe.akifuga profesa yupo bze tukifuga sisi niuchaf.shame upon you girl
 
Huwa siongei na Homosexual mlikosea Maisha Nazungumza Na Vijana Ambao bado wanatafuta ambao wanakutana Na Ma HR wakiwa hawana Ndevu.
 
Ndugu yangu kwa tuliopata kazi kwa kufuata mchakato wa sekreterieti ya ajira tunajua kuwa siku hizi hupaswi kuwa lelemama katika kufight ajira wewe kama umeajiriwa kwa ajira za mafungu kama za walimu na watu wa afya au kilimo ni heri utulie tu.
Ukikosea hupati kazi.
Hivi kwenye tangazo mmeshasema kuwa barua zote zipitie kwa meneja kwa anuani hii mtu anaandika barua kwa anuani tajwa ila anamtumia afisa manunuzi eti kisa yeye anaomba nafasi ya Afisa manunuzi msaidizi.
Ukimwambia aiandike upya anamind na vireasons vyake.
Tena si kosa hilo tu niliona makosa mengi ya kiuandishi ikiwemo kuweka sahii mahali palipopaswa kukaa jina na mahali pa kuweka sahihi yeye kuweka jina., Kujitambulisha yeye kama afisa
kwakuwa tu kasomea kitu fulani hata kabla ya kupata kazi.
Mkuu Vumilia vijana wa Jamii Forums ni wabishi Mtu alipata ajira ya Ualimu anataka Kulinganisha na Uhasibu.
 
Mhh mi naona hata kukomoana nako ni kwingi maana kutojua kuandika CV kunategemea yaweza kuwa kafundishwa hivi we unataka aandike kama unavojua, pia wasaili wengi wanatumia uhaba wa ajira kama fimbo ya kuwachapia watafuta kazi na kuonekana kama ni watu wasiojielewa, mi nilienda ofisi fulani HR aliyepewa kukaimu ni O level alivoiona CV yangu hakutaka hata kufanya usaili akaomba samahani naomba uendelee na shughuli zako hata hakusoma kilichomo
 
Mchongo mchongoma yote utafanya ila kumbuka mkono mtupu haulambwi pia kujua kupo japo kumekuw kwa siri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom