Ushauri kwa wanawake wote

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
4,040
8,895
1. Ukiona mpenzi wako hawezi kufanya mapenzi na wewe bila kuangalia picha za ngono ili avute stimu/hamu huyo achana naye. Yaani wewe humvutii wala hana hisia za kimapenzi na wewe ndio maana anaangalia video za ngono ili kuamsha hisia ila kama ni mumeo endelea naye maana huna jinsi ila ukae ukijua hana hisia na wewe.

2. Ukiona mpenzi wako anaona aibu kukutambulisha kwa marafiki zake au ndugu zake huyo achana naye. Huna mvuto wala hadhi ya kuwa mpenzi wake ndio maana anaona sooo marafiki zake kukufahamu. Hii ipo pande zote kwa wanaume na wanawake.

Kama ni mumeo au mkeo anaona aibu kukutambulisha kwa rafiki zake na wafanyakazi wenzio basi vumilia tu, huna jinsi, ila kama ni mpenzi tu au mchumba kaa naye mbali.

3. Tafuta au olewa na mpenzi unayevutiwa naye. Usiolewe na mtu kwa sababu na wewe unataka cheti cha ndoa. Ni aibu kuolewa na mtu ambaye huwezi kumtambulisha mbele za watu. Pia unadhani yeye anajisikiaje pale ambapo humtambui kama mumeo kwa rafiki zako na marafiki zako?

NB: Ushauri tu, haya mambo tunayaona sana mtaani na maofisini hasa mijini. Huko vijijini na mikoani watu hawana huo ujinga mume ni mume tu hata awe mfupi kama Emolo watu wanamtambulisha tu. Na mke ni mke tu hata awe na sura kama Remmy Ongala watu wanajivunia tu.
 
Back
Top Bottom