Ushauri kwa vijana wenzangu

Ushauri kwa vijana wenzangu

singojr

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2014
Posts
5,314
Reaction score
6,896
Jamani tufanye kazi.

Hakuna serikali au mtu atakayekuletea mafanikio bila kufanya kazi.

Vijana tumekumbwa na pepo la malalamiko. Kila kitu tunalaumu, tunalaumu wazazi, viongozi, elimu tuliyopewa, tunalaumu wenzetu wakifanikiwa.

Tutoke nje ya malalamiko, tujitazame tumefanya nini kubadili hali zetu.

Nchi yetu ni nzuri ina fursa nyingi za kujiendeleza. Kuna vijiji unapata hata acre 5 kwa laki moja. Tuna soko kubwa la ndani kwa bidhaa yoyote itakayozalishwa kwa umakini.

Tuache mambo ya kulaumu laumu tu.

Wanaokuambia biashara ngumu serikali haiwaangalii wanaoanza na mtaji mdogo wao walianzaje? Kwanini wewe usianze kama wao?

Wanalalamika bei ya mbolea lakini wanalima, kwanini na wewe usilime?

Unalalamika hakuna ajira lakini wapo wanaoajiriwa?

Wenzako wanaendelea,wanaanza maisha wanajenga, wanaongeza vipato wanakuwa na familia bora wewe unaendelea kulaumu tu.

Mwisho umefeli kimaisha story yako kwa kizazi chako itakuwa ni ipi? Serikali imenifanya niwe maskini au itakuwa pamoja na vikwazo vingi lakini bado nimetoboa.

Hakikisha hupotezi muda wako mwingi kwenye kulaumu wengine maana hutafanikiwa kamwe. Shauri huku unafanya kazi. Ukiona mwenzako kafanikiwa jifunze usianze kujiwekea dhania kuwa ni fisadi au nguvu za giza.

Hakuna heshima kwenye umaskini.
 
Ina maana hawafanyi kazi? Unataka kusema wanaofanyaa kazi hawalalamiki? Sasa Yale mabango ya mei mosi huwa ni ya nn?
 
Wale vijana Tuliokosa Ajira Tushazeeka na hatuwezi fanya kazi Nashangaa hawa vijana wa sasa wamerithi hadi hii shida yetu!
 
Ina maana hawafanyi kazi? Unataka kusema wanaofanyaa kazi hawalalamiki? Sasa Yale mabango ya mei mosi huwa ni ya nn?

Ile ni siku maalum, huwezi kuwa unalalamika mwanzo mwisho ukawa unafanya kazi vizuri
 
Kuna kijana mmoja alivuka mpaka hadi akaleta uzi eti wazazi wawape vijana urithi ama wawagawie mali..😂🤣
 
Nirahisi kusema unavyosema ila tambua wapo walioamua kuweka silaha chini wameshindwa kupambana
Siyo kila ardhi inachimbika kwa jembee
Kuusu kulalamika watu tutalalamika sanaa tuu sababu niwazi yapasa kupaza sauti juu ya yanayoendelea
 
We jamaa, Kama hujui nakujuza asilimia kubwa waliopo kwenye jukwaa la siasa ni watumishi

Wanaweza kuwa watumishi lakini ni wazembe ndio maana sijasema watumishi tufanyeni kazi. Mi nimeongelea wote soma vizuri
 
Nirahisi kusema unavyosema ila tambua wapo walioamua kuweka silaha chini wameshindwa kupambana
Siyo kila ardhi inachimbika kwa jembee
Kuusu kulalamika watu tutalalamika sanaa tuu sababu niwazi yapasa kupaza sauti juu ya yanayoendelea

Paza utawaambia wanaokutegemea kuwa umeshindwa maana ulikuwa unapaza sauti
 
Back
Top Bottom