Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,034
- 144,388
Huyu bwana mkubwa huenda ameshaanza kujirudi baada ya kuona anapingwa kila kona na sidhani Prof.Kabudi nae atakuwa hajamshirikisha katika hili.Profesa Palamagamba Kabudi anatafuta "...nitoke vipi!" Baada ya kugundua wanasiasa wanashindana na wasanii kutafuta kiki na followers instagram; na yeye tangu aingie bado hajapata kiki; ameona hii ndio fursa pekee ya kufuata nyayo za akina Bashite!!!
Kabudi anataka kutumia katiba mpya!!
Sizonje ameshasema katiba sio kipaumbele chake! Na pamoja na mapungufu kadhaa ya Katiba Pendekezwa; there's no way Sizonje ataitaka katiba inayotoa ruhusa ya kupingwa matokeo yake ya urais mahakamani hapo 2020 wakati ameshajiandaa kurudi tena kwa gharama yoyote ile!!!
Nawaambia kitu kimoja.Tungekuwa tuko tayari kuandama kwa gharama yoyoye ile kudai katiba ya Warioba wala nisingeleta huu ushauri ila kwakuwa sisi watanzania ni wazito kushinikiza watawala kutenda haki,basi ni bora hata hiyo katiba vinginevyo viongozi wetu wa upinzani wawe tayari kuongoza harakati za kudai katiba ya mzee Warioba kwa gharama yoyote ile.Hii inayo pendekezwa haitgkidhi mahitaji ya "WANAZENGO" Kwani ilishakuwa "BASHITERALIZED" tokea mwanzo. Kama wanataka katiba mpya walete rasimu ya WARYOBA
Ni nini kinachofanya uone amejirudi?! Kuamuru Nay wa Mitego aachiwe?!Huyu bwana mkubwa huenda ameshaanza kujirudi baada ya kuona anapingwa kila kona na sidhani Prof.Kabudi nae atakuwa hajamshirikisha katika hili.
Mambo gani hayo Kama kumsukuma mlevi?Leo nimeona magazeti mawili(Nipashe na HabariLeo) yanaongelea swala la kuanza tena mchakato wa kupata katiba mpya ambapo Nipashe linasema sheria kupitiwa upya ili kuwezesha mchakato huo.
Sitataraji kuwa hiyo habari itahusiana na siku ya wajinga maana imeandikwa na magazeti mawili tofauti.
Ushauri wangu kwa wapinzani ni bora kukubali mchakato huu uendelee kwa kumalizia na kura ya maoni ili tupate hiyo katiba mpya kwasababu kuu moja tu ambayo ni kupata fursa ya kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi.
Nashauri hivi kwasababu nakumbuka Katiba inayopendekezwa inatoa fursa ya kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi jambo ambalo tumekuwa tukilidai kwa muda mrefu.
TukipataTume Huru ya Uchaguzi itakuwa ni jambo la msingi sana na mengine yote yatafuata baadae ingawa naelewa bado kunaweza kukawa na changamoto ya kupata sheria nzuri itakayohakikisha kweli tunapata hiyo Tume Huru maana wabunge wengi bado ni wa CCM hivyo kunaweza kukawa na mvutano Bungeni katika kutunga sheria nzuri ya kuunda hiyo Tume Huru.
Pia Katiba mpya ikipatikana inaweza kupelekea kubadili au kutoa fursa ya kubadili sheria ya uchaguzi inayowatambua Wakurugenzi wa Halmashauri kama wasimamizi wa uchaguzi.
Na pia kama hii katiba mpya inatoa fursa ya kupinga mahakamani matokeo ya uraisi hii itakuwa ni fursa nyingine muhimu hivyo tukubali huu mchakato licha ya hawa CCM kuvuruga kwa kiasi kikubwa maoni ya wananchi katika kuandaa hiyo katiba mpya.
Tukifanikiwa kuingia madarakani au kupata wabunge wengi, mambo mengine yote itakuwa ni kama kusukuma mlevi.
Shida ni kukataa hiyo katiba inayopendekezwa alafu hakuna tunachofanya kushinikiza katiba ya mzee Warioba na uchaguzi ukija tutaanza tena kulalalimikia hii tume iliyopo kuwa si huru.Naunga mkono hoja,
Tnapaswa tulinganishe rasimu ya warioba, Katiba pendekezwa na katiba ya zamani.
Bado katiba pendekezwa ni nzuri zaidi ya katiba iliyopo, Ni pora kupiga hatua mbili au moja kuliko kutokupiga kabisa.katiba ya warioba bado ilikuwa na mapungufu mengi tu tukiacha ushabiki, Kwa heshima ya gharama ya pesa iliyotumiaka Tuanze na hii kwanza, baadae ndio madai mengine yaendelee
mimi shida ni kuzika hiyo pesa ambayo tuliitumia na naona hakuna mwenye uchungu nayo. Ni bora tuendelee tulipoishiaShida ni kukataa hiyo katiba inayopendekezwa alafu hakuna tunachofanya kushinikiza katiba ya mzee Warioba na uchaguzi ukija tutaanza tena kulalalimikia hii tume iliyopo kuwa si huru.
Tukataa hiyo katiba inayopendekezwa na tukashindwa kudai Tume Huru,basi tukubali matokeo.
Sometimes na sisi huwa hatujielewi.
Hapana hii habari ni ya kweli.Soma kupitia hii link:bashite deiiiiiiiiiiii1st april