Ushauri kwa UKAWA kuhusu Katiba Mpya

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Leo nimeona magazeti mawili(Nipashe na HabariLeo) yanaongelea swala la kuanza tena mchakato wa kupata katiba mpya ambapo Nipashe linasema sheria kupitiwa upya ili kuwezesha mchakato huo.

Kuisoma habari hiyo katika gazeti la Nipashe tumia hii link hapa chini:

Serikali yalainika hoja Katiba Mpya

Ushauri wangu kwa wapinzani ni bora kukubali mchakato huu uendelee kwa kumalizia na kura ya maoni ili tupate hiyo katiba mpya kwasababu kuu moja tu ambayo ni kupata fursa ya kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

Nashauri hivi kwasababu nakumbuka Katiba inayopendekezwa inatoa fursa ya kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi jambo ambalo tumekuwa tukilidai kwa muda mrefu.

TukipataTume Huru ya Uchaguzi itakuwa ni jambo la msingi sana na mengine yote yatafuata baadae ingawa naelewa bado kunaweza kukawa na changamoto ya kupata sheria nzuri itakayohakikisha kweli tunapata hiyo Tume Huru maana wabunge wengi bado ni wa CCM hivyo kunaweza kukawa na mvutano Bungeni katika kutunga sheria nzuri ya kuunda hiyo Tume Huru.

Pia Katiba mpya ikipatikana inaweza kupelekea kubadili au kutoa fursa ya kubadili sheria ya uchaguzi inayowatambua Wakurugenzi wa Halmashauri kama wasimamizi wa uchaguzi.

Na pia kama hii katiba mpya inatoa fursa ya kupinga mahakamani matokeo ya uraisi hii itakuwa ni fursa nyingine muhimu hivyo tukubali huu mchakato licha ya hawa CCM kuvuruga kwa kiasi kikubwa maoni ya wananchi katika kuandaa hiyo katiba mpya.

Tukifanikiwa kuingia madarakani au kupata wabunge wengi, mambo mengine yote itakuwa ni kama kusukuma mlevi.
 
Tunataka katiba yenye Maoni yetu sisi wananchi na si vinginevyo.... Kama sivyo bora wabaki nayo tuu.... Mimi nashindwa kuwaelewa wabunge wa SSM ambao hutumia wingi wao kufanya maamuzi ya kipuuzi kama walivyofanya 98 kupitisha sheria ya madini.... Ovyo kabisa hii mijitu
 
Tunaitaji katiba ya Warioba,katiba iliyobeba maoni ya wananchi na sio katiba ya Ccm. Kama hawawezi kutupa katiba tulio toa maoni bora ibaki hii ya kizamani.
 
Baba Bashite alisema, katiba sio kipaumbele chake kwa sasa. Back to the root hii nchi sio yake, as well as katiba sio yake ni ya watz kwa ujumla, hata gharama za kuiandaa ni kodi tunazolipa+mikopo(in turn wananchi ndo walipaji), hivyo hakuna namna kwa baba j kukataza kumalizika kwa mchakato wa katiba pendekezwa.

Note: tupaze sauti zetu katika hili.
 
kama katiba mpya irudishwe ya warioba na kubadili sheria ili isipitie bungeni,iundiwe kamati ya kuihakiki kisha wananchi waipigie kura
 
Profesa Palamagamba Kabudi anatafuta "...nitoke vipi!" Baada ya kugundua wanasiasa wanashindana na wasanii kutafuta kiki na followers instagram; na yeye tangu aingie bado hajapata kiki; ameona hii ndio fursa pekee ya kufuata nyayo za akina Bashite!!!

Kabudi anataka kutumia katiba mpya!!

Sizonje ameshasema katiba sio kipaumbele chake! Na pamoja na mapungufu kadhaa ya Katiba Pendekezwa; there's no way Sizonje ataitaka katiba inayotoa ruhusa ya kupingwa matokeo yake ya urais mahakamani hapo 2020 wakati ameshajiandaa kurudi tena kwa gharama yoyote ile!!!
 
Huyu bwana mkubwa huenda ameshaanza kujirudi baada ya kuona anapingwa kila kona na sidhani Prof.Kabudi nae atakuwa hajamshirikisha katika hili.
 
Hii inayo pendekezwa haitgkidhi mahitaji ya "WANAZENGO" Kwani ilishakuwa "BASHITERALIZED" tokea mwanzo. Kama wanataka katiba mpya walete rasimu ya WARYOBA
 
Kama anarudisha rasimu ya katiba mpya ya jaji Warioba ambayo yeye alikuwa mjumbe wa katiba hiyo nakubali, lakini kama anakuja na ile katiba fake ya Samweli Sitta big no!
 
Hii inayo pendekezwa haitgkidhi mahitaji ya "WANAZENGO" Kwani ilishakuwa "BASHITERALIZED" tokea mwanzo. Kama wanataka katiba mpya walete rasimu ya WARYOBA
Nawaambia kitu kimoja.Tungekuwa tuko tayari kuandama kwa gharama yoyoye ile kudai katiba ya Warioba wala nisingeleta huu ushauri ila kwakuwa sisi watanzania ni wazito kushinikiza watawala kutenda haki,basi ni bora hata hiyo katiba vinginevyo viongozi wetu wa upinzani wawe tayari kuongoza harakati za kudai katiba ya mzee Warioba kwa gharama yoyote ile.

Kama tumeshindwa hata kupigania haki ya kikatiba ya kufanya mikutano ya kisiasa hili la katiba ya mzee Warioba sidhani kama tutaliweza.

Hivi sasa hata juhudu tu za kudai Tume Huru ni kama vile hazipo na muda nao hautusubiri.
 
Huyu bwana mkubwa huenda ameshaanza kujirudi baada ya kuona anapingwa kila kona na sidhani Prof.Kabudi nae atakuwa hajamshirikisha katika hili.
Ni nini kinachofanya uone amejirudi?! Kuamuru Nay wa Mitego aachiwe?!

Binafsi naamini suala la kuamuru Nay wa Mitego aachiwe ni moja ya ushauri bora wa watu wake aliopata kuusikiliza vinginevyo angekuwa mjinga wakati picha mzima inaonesha wazi suala la who's Daudi Albert Bashite lingeibuka mahakamani kwavile ndilo ambalo limemuhusisha Rais moja kwa kwenye wimbo husika!!

Hivi inaingia akilini, leo hii anavitisha vyombo vya habari, tena mbele ya wageni na kuwaambia hawana uhuru wanaodhani wanao lakini siku mbili baadae anamwachia Nay wa Mitego kwamba ana uhuru wa kutoa maoni!!!!
 
Naunga mkono hoja,
Tnapaswa tulinganishe rasimu ya warioba, Katiba pendekezwa na katiba ya zamani.
Bado katiba pendekezwa ni nzuri zaidi ya katiba iliyopo, Ni pora kupiga hatua mbili au moja kuliko kutokupiga kabisa.katiba ya warioba bado ilikuwa na mapungufu mengi tu tukiacha ushabiki, Kwa heshima ya gharama ya pesa iliyotumiaka Tuanze na hii kwanza, baadae ndio madai mengine yaendelee
 
Leo nimeona magazeti mawili(Nipashe na HabariLeo) yanaongelea swala la kuanza tena mchakato wa kupata katiba mpya ambapo Nipashe linasema sheria kupitiwa upya ili kuwezesha mchakato huo.

Sitataraji kuwa hiyo habari itahusiana na siku ya wajinga maana imeandikwa na magazeti mawili tofauti.

Ushauri wangu kwa wapinzani ni bora kukubali mchakato huu uendelee kwa kumalizia na kura ya maoni ili tupate hiyo katiba mpya kwasababu kuu moja tu ambayo ni kupata fursa ya kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

Nashauri hivi kwasababu nakumbuka Katiba inayopendekezwa inatoa fursa ya kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi jambo ambalo tumekuwa tukilidai kwa muda mrefu.

TukipataTume Huru ya Uchaguzi itakuwa ni jambo la msingi sana na mengine yote yatafuata baadae ingawa naelewa bado kunaweza kukawa na changamoto ya kupata sheria nzuri itakayohakikisha kweli tunapata hiyo Tume Huru maana wabunge wengi bado ni wa CCM hivyo kunaweza kukawa na mvutano Bungeni katika kutunga sheria nzuri ya kuunda hiyo Tume Huru.

Pia Katiba mpya ikipatikana inaweza kupelekea kubadili au kutoa fursa ya kubadili sheria ya uchaguzi inayowatambua Wakurugenzi wa Halmashauri kama wasimamizi wa uchaguzi.

Na pia kama hii katiba mpya inatoa fursa ya kupinga mahakamani matokeo ya uraisi hii itakuwa ni fursa nyingine muhimu hivyo tukubali huu mchakato licha ya hawa CCM kuvuruga kwa kiasi kikubwa maoni ya wananchi katika kuandaa hiyo katiba mpya.

Tukifanikiwa kuingia madarakani au kupata wabunge wengi, mambo mengine yote itakuwa ni kama kusukuma mlevi.
Mambo gani hayo Kama kumsukuma mlevi?
 
Naunga mkono hoja,
Tnapaswa tulinganishe rasimu ya warioba, Katiba pendekezwa na katiba ya zamani.
Bado katiba pendekezwa ni nzuri zaidi ya katiba iliyopo, Ni pora kupiga hatua mbili au moja kuliko kutokupiga kabisa.katiba ya warioba bado ilikuwa na mapungufu mengi tu tukiacha ushabiki, Kwa heshima ya gharama ya pesa iliyotumiaka Tuanze na hii kwanza, baadae ndio madai mengine yaendelee
Shida ni kukataa hiyo katiba inayopendekezwa alafu hakuna tunachofanya kushinikiza katiba ya mzee Warioba na uchaguzi ukija tutaanza tena kulalalimikia hii tume iliyopo kuwa si huru.

Tukikataa hiyo katiba inayopendekezwa na tukashindwa kudai Tume Huru,basi tukubali matokeo.

Sometimes na sisi huwa hatujielewi.
 
Shida ni kukataa hiyo katiba inayopendekezwa alafu hakuna tunachofanya kushinikiza katiba ya mzee Warioba na uchaguzi ukija tutaanza tena kulalalimikia hii tume iliyopo kuwa si huru.

Tukataa hiyo katiba inayopendekezwa na tukashindwa kudai Tume Huru,basi tukubali matokeo.

Sometimes na sisi huwa hatujielewi.
mimi shida ni kuzika hiyo pesa ambayo tuliitumia na naona hakuna mwenye uchungu nayo. Ni bora tuendelee tulipoishia
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom