Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,843
Leo nimeona magazeti mawili(Nipashe na HabariLeo) yanaongelea swala la kuanza tena mchakato wa kupata katiba mpya ambapo Nipashe linasema sheria kupitiwa upya ili kuwezesha mchakato huo.
Kuisoma habari hiyo katika gazeti la Nipashe tumia hii link hapa chini:
Serikali yalainika hoja Katiba Mpya
Ushauri wangu kwa wapinzani ni bora kukubali mchakato huu uendelee kwa kumalizia na kura ya maoni ili tupate hiyo katiba mpya kwasababu kuu moja tu ambayo ni kupata fursa ya kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi.
Nashauri hivi kwasababu nakumbuka Katiba inayopendekezwa inatoa fursa ya kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi jambo ambalo tumekuwa tukilidai kwa muda mrefu.
TukipataTume Huru ya Uchaguzi itakuwa ni jambo la msingi sana na mengine yote yatafuata baadae ingawa naelewa bado kunaweza kukawa na changamoto ya kupata sheria nzuri itakayohakikisha kweli tunapata hiyo Tume Huru maana wabunge wengi bado ni wa CCM hivyo kunaweza kukawa na mvutano Bungeni katika kutunga sheria nzuri ya kuunda hiyo Tume Huru.
Pia Katiba mpya ikipatikana inaweza kupelekea kubadili au kutoa fursa ya kubadili sheria ya uchaguzi inayowatambua Wakurugenzi wa Halmashauri kama wasimamizi wa uchaguzi.
Na pia kama hii katiba mpya inatoa fursa ya kupinga mahakamani matokeo ya uraisi hii itakuwa ni fursa nyingine muhimu hivyo tukubali huu mchakato licha ya hawa CCM kuvuruga kwa kiasi kikubwa maoni ya wananchi katika kuandaa hiyo katiba mpya.
Tukifanikiwa kuingia madarakani au kupata wabunge wengi, mambo mengine yote itakuwa ni kama kusukuma mlevi.