bidam90
JF-Expert Member
- Aug 28, 2013
- 273
- 203
Kumekuwa na kasi ya ongezeko la uanzishwaji wa kozi mbalimbali katika vyuo vyetu Tanzania bila kuangalia ubora wa elimu kwa wanafunzi wanaomaliza (graduates) katika fani hizo, kuweza kushindana katika soko la ajira.Vyuo vyetu vimekosa ubunifu katika kufanya utafiti wa kozi husika kabla havijaanza kuifundisha hii inadhihirishwa wazi na kozi zilizotamba sana kipindi cha nyuma kama vile telecommunication eng. na computer science kwani vyuo vingi sana vilianzisha kozi hizi mwisho wake kuwaacha wanaomaliza kubaki mtaani bila kupata ajira au kukosa ubunifu wa kuweza kujiajiri katika fani hizo kutokana na mazingira ya ufundishaji wakiwa chuoni.
Kozi ya uhandisi wa mafuta na gesi (BSc PETROLEUM ENGINEERING) ni kozi ambayo inasikika sana kwasasa Tanzania kutokana na ugunduzi mkubwa wa gesi huko Mtwara.Kozi hii iliianza mwaka 2009/10 kwa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) na UDSM ikafwata kuIanzisha mwaka 2013/14.DIT nao wapo mbion kuianzisha.Napata wasiwasi juu ya kasi hii ya uanzishwaji wa hii kozi na nyengine zinazohusu mafuta na gesi katika vyuo vyetu bila kuandaa mazingira mazuri. Nashindwa kujua sijui ni shinikizo la serikali au maprofessa wa vyuo wenyewe.
Kumekuwa na changamoto nyingi SANA SANA katika ufundishaji wa kozi hii hapa nchini kwani ni kozi ambayo ni mpya na tofauti kidogo ukilinganisha na kozi nyengine kama vile za madini.Ni fani ambayo inahitaji sana kuwa na walimu wenye uzoefu wa mda mrefu katika masomo ,mazoezi mengi ya vitendo (Practical training, Internship),uelewa wa mambo mengi ya mafuta na gesi yanayotokea duniani hii ni kupitia kujifunza kwa watu wengine waliopo katika sekta hii mda mrefu nakusoma majarida,mijadala pia kujiunga na (organizations) mbalimbali kama vile Society of Petroleum Engineering(SPE).Ni tofauti kidogo na kozi za madini kwani zina wataalamu wengi walosomoea,pia upatikanaji wa maeneo ya kufanyia mazoezi kwa vitendo yapo.
Miongoni mwa changamoto zinazoikabili fani hii ya uhandisi wa mafuta (Petroleum Engineering) ni
-UKOSEFU WA WATAALAM (Lecturers): Walimu ni changamoto kubwa kwasasa kwani sio UDOM wala UDSM wote wanahangaika kutafuta walim wa kuweza kufundisha fani hio bila matumaini ya kuwapata.Wengi wanaofundisha kozi hii kwasasa ni walosoma Chemical engineering, Mechanical Eng. na geology) ambao hawana uelewa wa kutosha.Pia wengine bado ni wanafunzi wanaoendelea kusoma au kumalizia (masters, phd) zao nje ya nchi wanatumia mda wao wa ziada angalau kupunguza tatizo hili la walim.
-UKOSEFU WA MAENEO/KAMPUNI ZA KUFANYA MAZOEZI KWA VITENDO:Mazoezi kwa vitendo kama vile (practical training and internship) vinamsaidia mwanafunzi kupata (exposure) ya fani yake na kujua vitu vingine zaidi ya vile vya darasani.Makampuni mengi kwasasa yapo katika utafiti(Exploration) hivyo wanashindwa kuchukua wanafunzi kwa ajili ya field na hata ikichukua hawazidi wanafunzi wawili.Wengi wanaishiya kufanyia field maeneo ambayo hayaendani na wanachokisomea chuo mfano mwaka jana wanafunzi wengi walipelekwa kwe Viwanda vya nguo,TANESCO na hata wengine kukosa kabisa pa kwenda kufanya field.
-UKOSEFU WA MAABARA (PETROLEUM LABORATORIES)
Practicals zinamsaidia mwanafunzi kuweza ku (bridge theory and practice on various petroleum engineering aspects).Sio UDOM wala UDSM kwasasa wote hawana (labs) zinazohusiana na masuala ya (petroleum), angalau kidogo UDOM waliweza kupewa msaada wa mashine 3 (Distillation Unit, Ostwald type capillary viscometer and Ofite Lubricity Tester) na kampuni ya mafuta BG za kuweza kufanyia practicals katika kozi ya (Petroleum Lab 1 & 2) pamoja na hizo bado hazitoshi kuweza kumjenga mwanafunzi ki vile. Mwanzoni kozi inaanza ugunduzi wa gesi haukuwa mkubwa hivo UDOM wao walikuwa wakilipia gharama nyingi sana kupeleka wanafunzi kufanya practicals kwe labs zilizopo Mtwara (Schlumberger) ila kwasasa imekuwa vigumu kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi vile vile wahusika wa labs wanakosa mda kuwasimamia wanafunzi kutokana na kubanwa na kazi
-UPATIKANAJI WA (DATA) ZA KUFANYIA (PROJECTS)
Data upatikanaji wake umekuwa mgumu sana kwani makampuni inakuwa vigumu kwao kutoa data (confidential) wakati bado wapo kwe utafiti kutokana na ushindan uliopo wa makampuni mengi yanayofanya utafiti.Hii imepelekea wanafunzi watumie data za visima vilivyochimbwa miaka ya nyuma mwaka 1980.Ambazo visima vingi havikugunduliwa gesi (Dry/Brine wells).
- SAFETY CERTIFICATE
Ili uweze kufanya kazi baharini(offshore) unahitajika uwe na cheti cha usalama ambacho kukipata lazima uende Afrika kusini kuisoma hio kozi kwa mda wa wiki 2!Gharama za kusoma hio kozi ni kubwa sana kwa hali zetu ni vigumu kuisoma labda upate wa kukudhamini.Wengi wanamaliza kusoma bila kujua hata (Oil Rig) au shughuli za uchimbaji zinavyofanyika zaidi ya kuishia kujua (theory).
-UPATIKANAJI WA AJIRA
Sekta ya mafuta ni ngumu kuweza kujiajiri kwani inahitaji mtaji mkubwa sana ukilinganisha na sekta nyengine.Sio kwel kuwa ukisomea uhandisi wa mafuta na gesi una uhakika wa kupata ajira baada ya kumaliza chuo.Ni 15% tu ya wahandisi wa mafuta watakoajiriwa baada ya uzalishaji wa gesi kuanza mwaka 2022.Wengi watakaoajiriwa (85%) ni mafundi (Technicians) walosomea vyuo vya VETA ndo mana nguvu kubwa ya makampuni kwasasa ni chuo cha VETA Mtwara na (Diploma holders).
USHAURI
Ni vyema vyuo vyetu vikaanda mazingira mazuri ya ufundishaji kabla hawajakurupuka kuanzisha kozi, Ikiwezekana kuwepo na chuo kimoja tu kitakachotoa kozi flani mfano SUA masuala ya kilimo, pia kwa maoni yangu Ingekuwa bora ikabaki UDOM tu kufundisha masuala ya uhandisi wa mafuta kuliko kuwa na vyuo vingi wakati ubora wa elimu katika masuala ya mafuta Tanzania hauridhishi kutokana na mazingira yake. Hii ingekuwa rahisi hasa kwa serikal pamoja na makampuni kuweza kuelekeza nguvu zao katika kuchangia ujenzi na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali ktk chuo husika hapakuwa na haja ya UDSM nao kuanzisha hii kozi kwasasa kwani hali imezidi kuwa ngumu wanafunzi ni wengi,walimu hakuna,makumpuni bado hayajaanza kuajiri na kuchukua watu kwa ajili ya mazoezi kwa vitendo.