Ushauri kwa tunaoishi maeneo ya baridi kali

Ushauri kwa tunaoishi maeneo ya baridi kali

Darren2019

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2019
Posts
1,111
Reaction score
2,411
Kwa wale wa Njombe, Mbeya, Iringa, Arusha na ndugu zao ambao kiasili ni maeneo ya baridi bila shaka mtakubaliana nami kuwa msimu huu hali imekuwa mbaya kweli, mablanketi hayafui dafu.

Sasa kuna hii mbinu, pasha maji (siyo lazima yachemke km ya ugali), weka kwenye chupa za maji (hizi za plastic), funika vizuri, futa kwa kitambaa vizuri (kwa nje) ili kuhakikisha haina unyevu kisha weka kitandani kwenye shuka, unaweza kuwa na chupa mbili, tatu... inasaidia sana kutia joto kitandani hasa kwa wale wenye watoto wachanga, nilijaribu hii njia kupasha miguu na joto linadumu kwa muda mrefu sana.

Wale wa Dar na mikoa ya Pwani haiwahusu hii
 
20230708_194022.jpg
 
Back
Top Bottom