CK Allan
JF-Expert Member
- Aug 14, 2013
- 2,781
- 6,065
Binafsi nimefuatilia (ingawa sio kwa kina) soka la bongo na ligi yote inayoishia hivi karibuni (maana haijaisha kwa sisi wengine) napenda kutoa mapendekezo yafuatayo kwa TFF kama wanasikia watasikia kama hawatasikia basi...
1. RATIBA YA LIGI
Hili ni tatizo kubwa kwa kweli, yaani msimu huu na miaka yote ratiba ya mechi wanaijua TFF wenyewe, utakuta mechi zinasogezwa mbele au karibu kwa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu, niwaambie TFF ligi haiwezi kuwa bora kama ratiba haiheshimiwi! na mbaya zaidi kuna "namna" inafanyika katika kupanga nani acheze na nani na wapi na kwa wakati gani ili tu kumbeba fulani huu ni ujinga na soka litakufa...
2.KAMATI ZA UENDESHAJI LIGI
Nashindwa kuelelewa hapo TFF kuna kamati ngapi na zina uwezo gani! leo kesi ya simba bado haieleweki na kumbe kanuni ziko wazi kabisa!! mimi nashauri iwepo kamati moja tu!
Ikitoa maamuzi yawe hayo hayo, na pia kamati hiyo iwe na muda maalum wa kutatua matatizo ni ujinga kesi ya kadi tatu tu ichukue wiki mbili wakati ushahidi wote upo..
3. MATUMIZI YA VIFAA VYA MAWASILIANO KWA WAAMUZI
Niliona mara moja tu pale azam complex waamuzi wakiwa na vifaa vya mawasiliano, sijajua gharama zake na nishati inayotumika hadi TFF kushindwa kutumia vifaa vile kwenye kila mechi, pengine ujinga huu wa akina Martin Saanya wa kuruhusu magoli ya mikono pengine tusingeyaona.. kwani shida nini vifaa hivi visitumike?
4. WAAMUZI WA MECHI
Waamuzi na marefali lazima wapimwe kwa rekords zao za nyuma kabla ya kupewa kuchezesha mechi, kama ilivyo kwa watumishi wenye vyeti feki kadhalika na huku tunao waamuzi FEKI mfano mojawapo ni Martin Saanya, TFF inabidi iwachunguze na ikibidi kuwatangaza mapema kabla ya mechi ili ikibidi timu ziweke pingamizi mapema, wapo waamuzi ambao hata ndondo cup hawastahili kuchezesha lakini tunawaona ligi kuu, tafadhali sana jirekebisheni.
5. UPENDELEO WA KUTOA ADHABU KWA BAADHI YA TIMU NA WACHEZAJI
Wachezaji kama binadamu wengine hufanya makosa na inabidi kuwawajibisha bila kujali timu zao au hadhi zao, tumeona upendeleo wa wazi kwa baadhi ya timu, wengine wakiepewa adhabu na wengine wakiachwa, kuna tukio moja la hivi karibuni ambalo sijaona sana watu wengi wakilipa mkazo lakini kwangu mimi niliona ni uzembe wa wazi wa TFF kutochukua hatua kwa Calvin Yondan kwa kitendo alichomfanyia Mbaraka Yusuph, pamoja na kuwa kadi ile ilifutwa lakini Kelvin ilimpasa kufungiwa walau mechi moja!
Kwa wale ambao hawakuangalia ile mechi ni kuwa mara nyingi Kelvin alimfanyia rafu Mbaraka na mwishowe Mbaraka akaamua kulipizia na akapewa kadi nyekundu, sasa wakati anatoka ndipo Kelvin akawa ana mdhihaki kwa kumpa mpira huku akimwambia maneno ya kumkejeli kuwa "chukua mpira sasa ukacheze" hakika ingekuwa mimi ningeondoka na meno mawili ya kelvin, kumbuka Zidane alimpiga mtu kichwa kwa ujinga kama huu.
6. MECHI ZOTE ZIREKODIWE
Inashangaza kwa dunia ya sasa, eti kumbukumbu za vido za mechi iliyochezwa mwezi wa kwanza eti haipo, nashauri TFF mbali na kuitegemea AZAM TV, ninyi wenyewe muwe na vifaa vyenu vya kutunzia mechi kwa ajili ya kusolve kesi, mfano kwa tatizo hili la kadi tatu mgeweza kulimaliza ndani ya nusu saa tu iwapo kila mechi ingekuwa ianrekodiwa..
Naomba niishie hapo wadau wengine wataongezewa
By allan
Mdau wa soka.