Ushauri kwa TBC 1 juu ya usomaji wa Taarifa ya Habari

evonik

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
3,998
5,150
Habari Jf!!!

Kutokana na dhoruba ya Azam TV kupandisha vifurushi vyake pamoja na kukata local channels zote na kuacha TBC pekee na ile ya kwao extra, sasa nimekuwa mfuatiliaj mzuri wa TBC 1, hususani taarifa ya habari saa mbili usiku.

Iko hivi, taarifa ile ya habari husomwa na wasomaji wawili ambapo mara nyingi huwa ni jinsia mbili tofauti yaani KE na ME, sasa Hawa wasomaji,(watangazaji) husoma taarifa moja wote kwa kupokezana kwa wakati mmoja na wakati mwingne husubiriana kwa Muda yaani kila mmoja kujichanganya kumsubiria mwenzake, kama hiyo haitoshi cameraman huweza kutokea kumchukua ambaye hasomi taarifa kwa wakati huo na kumuonesha kwa sekunde kadhaa, kama hiyo haitoshi wakati mwingne hujadiliana wao kwa wao kuhusu taarifa fulani

Athari ambazo husababishwa na watu wawili Kusoma taarifa moja ni

1) Inapoteza Muda taarifa mbili kusomwa na watu wawili, kumbuka Kuna dk 30 za kusoma habari za kitaifa.

2) Inapoteza concentration ya watazamajj wa habari sababu huyu hajamaliza kusoma kadakia mwingine.

3) Wakati mwingne humchanganya cameraman kujua ni yupi ataongea.

4) Hupelekea kuwepo kwa taarifa chache zinazoripotiwa

Mnaweza kujifunza kwa wengine ambao husoma mtu mmoja na taarifa inakuwa nzuri yenye kuvutia Zaidi.

Ni hayo tu.

NAWASILISHA WAKUU....
 
Halafu watangazaji wenyewe sio mahiri katika kufanya tafiti kabla hawajaingia chumba cha habari. Wanaongea vitu vya kawaida sana na kuulizana mambo yasiendana na habari iliyoko mezani. Kama wangekuwa wanaangalia TV za Kenya sidhani kama hawa watangazaji wangekubali kutangaza, watangazaji wa Kenya utafurahi kuwaangalia, wana vitu vingi vinavyovutia watazamaji.
Kwa kweli hawa jamaa wa TBC wanakuwa kama wamelazimishwa kutangaza, hawana ari wapo wapo tu! Kwa jinsi walivyo wanatakiwa wajitume sana ili kuendana na ushindani wa soko.
 
Toka waharibu mudi yangu walivyokuwa wanapendelea upande Fulani kusoma Magazeti, sidhani kama naweza kuangalia tena TBC1.
 
Ata ivyo una moyo wa uvumilivu sana... Yani unakaa kabisa kuangalia tbc!... Tena una washauri kabisa.. Hongera aisee.... Hao na mwenzao star tv sifaamu hata kama wapo kwenye kingamuzi changu
 
tbc vipindi vyao havieleweki wanakatisha tu ovyo. ile tamthilia ya mao doudou wameishia kati na hawajaonesha tena...hawa jamaa wanaboa kweli.

kinachowapa jeuri TBC ni kutofanya biashara ndo maana taarifa zao au vipind vyao haviendani sambamba na soko la laeo
 
Halafu watangazaji wenyewe sio mahiri katika kufanya tafiti kabla hawajaingia chumba cha habari. Wanaongea vitu vya kawaida sana na kuulizana mambo yasiendana na habari iliyoko mezani. Kama wangekuwa wanaangalia TV za Kenya sidhani kama hawa watangazaji wangekubali kutangaza, watangazaji wa Kenya utafurahi kuwaangalia, wana vitu vingi vinavyovutia watazamaji.
Kwa kweli hawa jamaa wa TBC wanakuwa kama wamelazimishwa kutangaza, hawana ari wapo wapo tu! Kwa jinsi walivyo wanatakiwa wajitume sana ili kuendana na ushindani wa soko.
Kuna kipindi cha Nipashe kinaonyeshwa Citizen Tv ya Kenya ni sehem nzur ya wao kujifunzia.
 
Halafu watangazaji wenyewe sio mahiri katika kufanya tafiti kabla hawajaingia chumba cha habari. Wanaongea vitu vya kawaida sana na kuulizana mambo yasiendana na habari iliyoko mezani. Kama wangekuwa wanaangalia TV za Kenya sidhani kama hawa watangazaji wangekubali kutangaza, watangazaji wa Kenya utafurahi kuwaangalia, wana vitu vingi vinavyovutia watazamaji.
Kwa kweli hawa jamaa wa TBC wanakuwa kama wamelazimishwa kutangaza, hawana ari wapo wapo tu! Kwa jinsi walivyo wanatakiwa wajitume sana ili kuendana na ushindani wa soko.
Ina maana hakuna watangazaji wengine kwenye tv za Tanzania mpaka utolee mfano kwa hawa tunaogombea bomba la mafuta?
 
Hivi kuna watu bado mnatazama TBC ni bora kusikiliza TBC Taifa fm au RTD kuliko tbc tv jamaa wamebweteka nafikiri kwa sababu uhakika wa salary upo kwa ajili ya kodi zetu
 
Hata sipotezi muda kucheki huo mchanel hovyo kabisa! King'amuzi kikikata ni heri kuzima tv na kulala loh!
 
Back
Top Bottom