Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,673
- 149,860
Baada ya nchi nyingine wahisani kuungana na Marekani katika kusitisha misaada,naona itakuwa vigumu sana kwa serikali kupuuza jambo hili licha ya kauli za kujitutumua kuwa tunaweza ku-manage kuendesha nchi bila misaada ya wahisani.
Huenda tunaweza lakini tatizo ni kuwa hatukujipanga na tunahitaji muda kujipanga na muda huo kwa sasa haupo kwani tumeshachelewa.
Hivyo,kwa mtazamo wangu,naishauri serikali kuunda kitu kinachoitwa "Goverment Negotiating Team" kwenda kuonana na nchi wahisani kutafuta suluhu ya mgogoro huu.
Kwa sasa tunaweza kuweka msimamo wa kuachana na bwana wakubwa hawa ila wakati utafika tutajikuta tunakwama na tutapaswa kuwarudia kwa aibu unless serikali ichukue hatua za dharura kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kuanzia Ikulu mpaka kwenye ofisi ya Mtendaji wa Mtaa.
Hata hivyo,tukumbuke tuna changamoto za kuandaa uchaguzi wa serikali za mitaa,deni la Taifa,milioni 50 kwa kila kijiji,elimu bure,kura ya maoni au kuanza upya kwa Bunge la katiba, fedha za kuendesha Bunge la Bajeti,n.k.Tusipokuwa makini tutajikuta hakuna miradi ya maendeleo inayofanyika au kukamilika.
Timu hiyo ya Wataalamu inaweza kuundwa na watu wafuatao;
1.Raisi Mstaafu Kikwete(mwenyekiti wa jopo)
2.Waziri wa Mambo ya Nje
3.Waziri wa Fedha
4.Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
5.Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi
6.Waziri wa Sheria
7.Katibu Mkuu Wizara ya Sheria
Raisi Mstaafu Kikwete anafaa zaidi kwasababu amekuwa karibu sana na wazungu hawa katika kipindi cha uongozi wake hivyo anaweza kuwa na msaada zaidi katika jambo hili kama mwenyekiti wa Jopo.
Hao wengine kwa nafasi zao wanahusika moja kwa moja na swala hili.
Waziri wa Sheria na Katibu wake Mkuu wanaweza kuhusishwa katika Timu kama watu watakaohusika kutoa ufafanuzi(commitment) ya serikali kuhusu kupitia upya Sheria ya Makosa ya Mtandao.
Watu wengine wanaoweza kuwepo kwenye Timu hii ni mwakilishi wa serikali ya Zanzibar na mwakilishi wa vyama vya siasa ambao watakuwa na wajibu wa kueleza commitment ya serikali ya Zanzibar na Vyama vya Siasa katika kumaliza mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar.
Mwisho,jambo hili liwe funzo katika kuendesha chaguzi zetu na zaidi iwe funzo la sisi kujitegemea kwa kubuni na kusimamia vyanzo vyetu vya mapato na kuachana kabisa na mawazo ya kutegemea wahisani.
Lazima nikiri kuwa ni aibu na fedheha sana kuishi kwa kutegemea misaada lakini ni aibu na fedheha zaidi kubembeleza misaada lakini pia lazima tujiulize tumefikaje hapa na tunatokaje.