USHAURI KWA SERIKALI KUPITIA KWA WAZIRI WA ARDHI TANZANIA

MWAKISALU

Senior Member
Nov 1, 2013
100
46
Namshukuru sana mwenyezi Mungu kwa kuendelea kutupa uzima na afya njema.

Pia napenda kuchukua nafasi hii kuwatakia mfungo mwema wenzetu wote walio ktk mifungo mbalimbali kwa imani zao.

Mheshimiwa waziri wa Ardhi mhe Lukuvi, awali ya yote nakupongeza kwa kuwa u mtu makini na unafanya kazi zako vizuri sana.

Kwa kumbukumbu zangu nakumbuka ushauri huu ninaokusudia kukushauri leo niliwahi kumshauri Prof Tibaijuka akiwa waziri wa ARDHI lakini sikuona lolote likifanyika sijui pengine hakuona umuhimu wa hoja yangu.

Mhe waziri ushauri wangu kwa serikali kupitia wizara yako ni kuhusu mipango miji.

Miji na majiji yetu karibu yote yapo ktk squatter. Na kwa kuwa miji inakuwa nakushaurini kwamba achaneni kwanza na kuhangaika kurekebisha mijini ambamo tayari miundombinu yake ilikosewa tangu mwanzo nendeni kapangeni miji maeneo ambayo watu wanakimbilia kujenga ili sasa mkipanga huko mdipo mrudi kuhangaikia kurekebisha mijini.

Ikiwa mtakomaa kurekebisha mijini mkasahau kurekebisha maeneo yanayokua mtakuwa na kazi nzito sana hapo baadaye kurekebisha eneo kubwa lililoharibika. Nitoe mfano wa jiji la dar mnaweza kwenda kupanga miji huko chanika, kigamboni, mbweni kibaha nk ili watu waishi ktk maeneo yanayoeleweka na yaliyo planned.

Ghalama za kureblkebisha mjini uliopangika vibaya ni kubwa sana kuliko maeneo mapya. Nashauri hata kama hamtapima maeneo hao ninyi choreni mpangilip wa barabara tu zinazoeleweka. Na wambieni vingozi wote wa serikali za mitaa wasimamie jukumu hilo maana wao ndiyo wanaishi na jamii huko mitaani.


Barabara kama zitachorwa au kuanishwa ktk maeneo ambayo miji inakua itasaidia sana kuleta muonekano wa miji vizuri. Ikiwa hamtafanya hivi ninavyowashauri basi jueni kuwa serikali itabaki kupoteza hela nyingi kufidia watu pale ambapo inataka kurekebisha mipango miji.

Na ili mfanikishe hili wapeni semina viongozi a serikali za mitaa kwamba kila panapotokea uzwaji wa eneo lazima afisa ardhi au mipango miji awepo. Lakini isiwe ni kigezo kuwasumbua wananchi kiwalipa hao maofisa wenu. Hii liganywe ni moja ya kazi za ofisa ardhi za kila siku.

Natumaini mtasoma ujumbe wangu na mtaufanyia kazi kwa mustakabali wa nchi yetu

Ndimi Lutengano Nkanda Mwakisalu_+255784636261
 
Back
Top Bottom