Ushauri kwa ripota wa rais ikulu (Kurugenzi ya habari ikulu)

makaa

Member
Dec 13, 2016
21
15
Nimefatilia hotuba nyingi za mheshimiwa Rais JPM akiwa kanda ya ziwa katika hotuba zake kwa wananchi huwa anatumia lugha za asili ya makabila ya huko.

Nashauri wanao ripoti habari hizi hasa zile video zilizowekwa katika social media kama youtube.com wangekuwa wanatasfiri zile "vurnecular language" kwa kutuwekea sub titles za kiswahili.

Kiongozi wa nchi anaweza kutoa taarifa au ufafanuzi wa jambo lihusulo maslahi ya nchi akiwa katika ziara zake sehemu yeyote nchini. Mfano; Ishu ya tanesco kupandisha bei ya umeme kuanzia 01.01.2017 Mheshimiwa aliitolea ufafuzi akiwa Kagera.

Nafikiri ni haki ya Watanzania kuelewa zile vernacular language.
 
Ahsante kwa ushauri mkuu.

Japo kwenye mitandao ndo sehemu pekee ambayo hata mtu ambaye hakuwahi kuuona ule ubao mweusi anaweza kumshauri professor.
 
Ahsante kwa ushauri mkuu.

Japo kwenye mitandao ndo sehemu pekee ambayo hata mtu ambaye hakuwahi kuuona ule ubao mweusi anaweza kumshauri professor.
Kuwa profesa sio kigezo cha kujua kila kitu, unaweza pewa ushauri na mtu yeyote hata huyo uliyemtaja hapo.
 
Back
Top Bottom