Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,265
- 21,442
Tukiweka ushabiki wa kisiasa pembeni, lazima tutakiri kwamba kwa sasa mambo Tanzania yako mrama sana, si tu katika siasa bali pia uhusiano wa serikali na wananchi wake. Rais Magufuli ana nia nzuri, lakini mengi ya anayotenda yanaonekana na wengi kuwa yasiyo na faida tu. Na ukweli ni kwamba staili ya uongozi ya Magufuli ya u-bulldozer inaonekana kama sio jambo lenye kufurahisha sana.
Wasiwasi uliopo sasa ni kama Tanzania ni volkano inayokua kila siku. Kuna siku tutaona mlipuko?
Ningependa kumshauri kwa nguvu zote Rais Magufuli kwamba amuombe Prof. Mwandosya kuwa mshauri wake katika uendeshaji serikali. Najua wazi kwamba "there is no love lost between Prof. Mwandosya na Rais Magufuli", lakini kwa ajili ya faida ya Tanzania, ningemsihi Rais Magufuli atafakari sana juu ya hili. Rais Magufuli ni bulldozer linalohitajika sana kuirekebisha Tanzania, lakini pia ni bulldozer linalohitaji mshauri makini kama Prof Mwandosya.
Ningependa kumkumbusha Rais Magufuli ukweli kwamba, japokuwa Raisi Kikwete alikuwa na issue zake pia dhidi ya Prof. Mwandosya, lakini alikuja kutambua busara na hekima zake na kumleta karibu sana naye (japo in a cunning manner) katika kuendesha serikali, na mambo mengi ya serikali yakafanikiwa kutokana na busara za Prof Mwandosya. Rais Magufuli analijua hili. Raisi Magufuli amuulize pia rafiki yake Mkapa juu ya busara za Prof. Mwandosya kama mshauri wake. In fact, between Mkapa na Mwandosya kama washauri - I would go for Mwandosya!
Kwa hiyo Rais Magufuli, mwite Prof. Mwandosya kutoka huko kijijini aje awe mshauri wako mkuu, na umsikilize atakachokushauri. Prof. Mwandosya ni mojawapo wa watu wachache sana Tanzania ambaye atakushauri bila umbea au kujipendekeza.