vevenononombo
JF-Expert Member
- Jun 19, 2015
- 1,289
- 420
Nakuja mbele yenu wana jamii forum kwa niaba ya rafiki yangu kipenzi ambaye sio mpenzi wa mitandao ya kijamii,Ni kijana chini ya miaka 30,msomi wa elimu nzuri ya kiwango cha uzamili akiwa na kazi nzuri na maisha yanaenda vizur,ajaoa ila amekumbana na mambo kadhaa yanayomfanya aombe ushauri kwa watu juu ya yaliyomkuta,Alikuwa na gf wakati huo wakiwa wamemaliza kidato cha sita ,wakiwa mwaka wa kwanza binti akapata ujauzito na wakakubaliana kulea mimba kwa siri kubwa hadi hapo mimba itajapikuwa kubwa lkn wakiwa ktk mpango wao huo wa siri mimba ikiwa imefikisha miezi mitatu yuke mpenzi wake akapata ajali akiwa bafuni na kupoteza faham hivyo kukimbizwa ktk hospital moja ya kijeshi jijin DSM ndipo siri ikagundulika kuwa binti alikuwa na ujauzito na ujauzito ule uliharibika,na mimba ile ilifanya rafiki yangu huyo kutoelewana na familia ya binti huyo kwani waliona anamwalibia maisha mtoto wao hivyo kumuonya kutokuwa na mahusiano tena na binti yao,huo ukawa ndio mwisho Wa mahusiano yao,maisha yakaendelea baada ya kumaliza Chuo mwaka mmoja baadae alikutana na binti mrembo sana kutoka kanda ya kaskazini walipendana akiwa na malengo ya kumuweka ndani ktk mambo yakuonjana binti kapata ujauzito ikawa habar njema sana kwa rafiki yangu huyo,binti akiwa anarudi kwao akapata ajali na kupiteza ule ujauzito tena ulikuwa ni Wa mapacha,hali ile ilimchanganya sana rafiki yangu mpaka kuanza kuamini kuwa binti yule aliitoa ile mimba lkn binti aliendelea kusisitiza kuwa ile ajali aliyopata ndio ilipelekea mimba kutoka na kiukweli alilazwa siku kama nn mfululizo,