Ushauri kwa madakatari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa madakatari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by meeku, Jun 29, 2012.

 1. meeku

  meeku JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 571
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwanza nianze kuwapongeza madaktari kwa kazi nzuri waliyoianza. Ni wazi kuwa kazii hii ikifanikiwa vyema itaokoa maisha ya watanzania wengi ambao hawana fedha za kutibiwa Apolo. Anayeona kuwa madaktari wanafanya vibaya basi vyema akaelimishwa.

  Ni ajabu kuambiwa kuwa hospitali za serikali zina City scan moja tu iliyopo Muhimbili na ambayo imeharibika miezi saba iliyopita. Ni aibu kwa taifa ambalo viongozi wake wanazii kujilimbikizia mali kila kukicha huku wananchi wakifa kwa kukosa matibabu stahiki. Kwanza ni machungu ya muda na wananchi tunapaswa kuunga mkono juhudi hizi ili kuwajibisha viongozi hawa ambao kwa lugha rahisi tunaweza kuwaita "majizi".

  Ombi langu. Wananchi tuunge mkono juhudi za madakatari na zifanyike juhudi za kuchangia ili mwanamapinduzi kiongozi r. Ulimboka apate matibabu na aweze kurudi kwenye vita. Lakini wapo madaktari ambao wameanza kutolewa kafara. Ningeomba zifanyike juhudi za maksudi ili wachangiwe chochote cha kuwafanya waendelee na mapambano. Hizi ni mbinu za kudhoofisha na ni vyema tuwe nao pamoja. Leteni namba za Tigo pesa na M-pesa tuchangie.

  Tatu Dr Ulimboka aenziwe kwa mchango wake na ikibidi historia iandikwe.

  naomba tujiulize ufisadi ni kiasi gani umefanyika hapa nchini ambao ungekomboa nchi hii. Ni aibu kwa viongozi wa nchi hii.

  Noamba kuwakilisha.
   
 2. L

  LIALIA Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Nakubaliana na wewe kabisa, hii serikali lazima ipewe somo na hii ndo namna pekee, madaktari sio wajinga na lengo lao sio kukomoa wananchi. Kitu cha msingi madaktari wanatakiwa waielimishe jamii na wanchi wa nchii hii walio wapole kama kondoo siku zote kuwa wanawapenda na lengo sio kuwakomoa. Dr ulimboka anagoma si kwamba hajui kuwa babu yake huko mbeya ataathirika na mgomo, La hasha, lengo ni kutetea maslahi na si kuumiza mwanachi wa kawaida kule kijijini
   
 3. meeku

  meeku JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 571
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  NASHUKURU KAMA NIMEELEWEKA. nA NDIYO MAANA NADHANI MADAKTARI LICHA YA KUFANYA JEMA HILI WANAYO KAZI YA ZIADA KUWAELIMISHA WANANCHI KWANI SIASA INATUMIKA KUWAHADAA. LAKINI PIA SISI WANANCHI TUJITAHIDI KUELIMISHANA KUHUSU MGOMO HUU. NI WAZI KUWA SERIKALI YETU NI DHALIMU NA WALA MTU HAITAJI ELIMU KULIJUA HILO. ZAIDI NIOMBE KILA MTANZANIA KWA DINI YAKE AOMBE ILI TUFANIKISHE KUPATA UKOMBOZI
   
Loading...