Ushauri kwa huyu kaka

bwii

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2014
Posts
1,432
Reaction score
2,679
Salaam zenu wandugu

Kuna jamaa yangu anatatizo moja linamsumbua anaomba msaada wa kimawazo toka kwangu,hivo nami bila kusita nmeamua kulileta kwenu ili tuweze kumsaidia sababu humu najua kuna wajuz wa mambo.Huyu jamaa yangu anaishi maeneo ya uswazi kidogo ni mkimya pia na hana stori nyingi na watu wa mtaa huo japo ana kama mwaka na nusu.

Moja ya sifa zake ni anapenda sana wanawake ila hachukui wanawake wa mtaa huo na mara nyingi anajua anapofanyia mambo yake japo mara chache huwapeleka wanawake chumbani kwake ila ye mwenyewe anasema sio watu wake sababu kuna kipindi alikua anajiendeleza kimasomo hivo anasoma nao na ni stor na kucheki muvi ndo shuhuli kubwa sanasana pia ilikua mnywaji kama sio mlevi ila kwa sasa kaacha na kaamua kutulia.

Kama wiki mbili zilizopita kaamua kuishi na mwanamke wake ambaye hata sisi tunamjua(mchumba wake)ila tatizo ni kwamba majiran wameanzisha shari na huyu mwanamke wake (huyu binti na mpole na mstaarabu sana)
kisa ni kua kuna bomba la jumuia karibu na anapoishi (siunajua mambo ya uswazi tenaa)alikua anapiga stor na mwanamke mwingine.

Ila akatokea mwanamke ambaye pia ni jiran(hawa wanawake hawaivi)na kuanza kuntukana mchumba wake matusi yanguoni na kumwambia wao ndo wenye mtaa na ni malaya tu.Jamaa kuja kuambiwa alitulia tu sababu huyu aliemtukana katoka kufiwa na mme wake hivi karibuni hivo jamaa kama hapend kumwambia chochota kakaakimya tu.na sasa bado wakikutana bomban anazidi kumtukana na kufanyia visa.

Jamaa ndo kaja kuniomba ushaur sababu hayo mambo yanamkera.Ila anaogopa kumvaa huyu mwanamke anaye mtukana mwanamke wake hadi anataka siku amnywe tungi ili atoe machungu yake.ila kwa nnavomfaham ni mkorof sana pindi alipokua anakunywa pombe kwa yeyote anayekorofishana nae.

Je tunamshaurije
 
Hasa huyu si wa kumpeleka kwa mjumbe tu, apewe maneno yake akae chini atulie, na pia kujitolea lawama siku ukimlamba vibao kesi isiwe kubwa
 
Mambo ya wanawake waachie wanawake,na usiamini kila jambo analokueleza mwanamke,utapata aibu ya mwaka...
 
Inaonekana Huyo Mwanamke Anaemtukana Mwenzie Alikua Na Mpenzi Wake Wa Zamani.Na Ndomana Anajiamini Kiasi Hicho.Ila Mwanaume Lijari Hawezi Kushindwa Kumaliza Inshu Ndogo Kama Hiyo.
 
Kisa cha kutukanwa ni nini........?.......funguka mkuu.......mambo ya uswazi tunayajua........si bure kuna kitu.......
Btw.....kwa nini umuandikie mwenzio......yeye ni mkoma.......?.........
 
Amnywee hizo bia akamtukane live kuna mijamke ya mitaani ni shidaaa inachokoko kweli ikiona haitongozwi inakuwa na wivu na watoto Wa watu bila sababu na atukanwe hasa hata wazoea tena.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…