Makamanda People's!
Kuanzia sasa kuna miaka 2 kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa/Vijiji, pia kuna miaka 3 kuelekea uchaguzi mkuu.
Nashauri yafuatayo yafanyiwe kazi;
(1) Mfumo wa ujenzi wa Misingi uboreshwe sana na usimamizi wake ufanyike ikiwezekana kuwe na kitengo ambacho si rasmi sana cha kuwepo Walezi wa Kata ambao watafanya ufuatiliaji kujiridhisha kama Misingi imeundwa kila Kitongoji.
(2) Kuwajua/kuwaandaa mapema watia nia watakaogombea nafasi mbalimbali kwenye Serikali za Mitaa ili kupata muda wa kuwapima uwezo wao na namna wanavyoshiriki kukijenga Chama.
(3) Kuwajua Mapema Watia nia watakaogombea Ubunge ili waweze kushiriki kwenye ujenzi wa Chama, pia wanachama wapate nafasi ya kuwafahamu mapema na kuwapima kuona nani anafaa kuwa Mgombea Ubunge mwaka 2025 katika Jimbo husika.
(3) Chama kitafute kila mbinu kuhakikisha kinawasapoti kwa kiasi cha fedha wagombea wakati wa uchaguzi.
Huko tuendako kuna kila dalili za kutokupata Wagombea wengi Ngazi za chini hususani Wagombea Uwenyeviti wa Vijij/Mitaa na Wagombea Udiwani kutokana na Chama kuwatelekeza.
(4) Kuweka utaratibu mzuri na rahisi wa kusajili Wanachama (Chadema Digital) kwa kuhakikisha kila Jimbo/Wilaya kunakuwa na Mtambo (Mashine) wa kutengeneza kadi za kielekitroniki, vinginevyo zoezi litakuwa gumu maana hata wale waliojisajili na kulipa Ada za Uanachama kwa kiasi kikubwa hawajapata kadi zao kutokana na mashine hizo kupatikana ngazi za Kanda.
Jambo hilo linadumaza mchakato wa usajili wa kielekitroniki (Chadema Digital).
(5) Chama kione umhimu wa kupunguza gharama zisizokuwa za lazima kwa kuvunja uongozi wa KANDA ambao kimsingi kazi yake haionekani.
Maafisa wa Kanda wamepewa usafiri, wanalipwa na kazi hawafanyi, fedha zinazotumika kwenye Kanda zingeshuka chini kujenga Misingi Chama kingekuwa mbali sana.
Nawasilisha.