Ushauri kwa CCM: Kubana matumizi katika Chama kusifananishwe na ilivyo serikalini: Chama ni "Hiari"

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
4,005
3,643
Nimefuatilia mabadiliko yanayoendelea ndani ya Chama chetu. Mengi yana nia njema kwa Chama ila nashauri uangalifu uwepo. Hoja zijengwe,zijadiliwe kwa kina,na ziridhiwe bila chembechembe nyingi za mashaka. Ninaamini katika Demokrasia ya kweli! Moja ya nguzo kubwa ya ukomavu na uendelevu wa Chama cha siasa ni Demokrasia . Tofauti na hapo, Uongozi unaweza kuwa na maono mazuri,ila yakawa na approach mbaya ,yasikubalike kwa wengi. Ukizingatia uanachama ni hiari, ni vyema kuweka element ya ushawishi wa hoja kwa kila jambo lenye kuleta mabadiliko na likubalike kwa hiari na Wanachama ndani ya matakwa ya katiba.
Ninajua,Serikalini ni kinyume,itakavyoamuliwa ngazi za juu, ndivyo itakuwa. Nafasi ya kujadili ni finyu.
Katika Chama,ukisema unabana matumizi,unapunguza wajumbe,uwe na hoja ya sababu na ijadiliwe. Mfano,ndani ya Chama kuna wenye mawazo ya kupanua vitega uchumi na mapato ya Chama,wanaona fursa kuwa zipo. Hawa hawataona haja sana ya kupunguza wajumbe kwa kigezo cha gharama! Wataona wajumbe wengi ni mtaji wa kusimamia vitega uchumi vitakavyoongezeka! Na pia,wakiwa wengi watapanua wigo wa Chama,kwani lengo ni kukuza zaidi chama Strategically. Hata katika Serikali, kama ni kweli,hatujapunguza Mawaziria au Mikoa tulipoamua kubana Matumizi. Ila tumepunguza posho,vikao n k, ambapo sasa ufanisi wa utendaji (na mapato) inasemekana vimeongezeka.
Pia nashauri,tuwe na sababu vivid na pubicly justifiable tunapotaka kufukuza mwanachama! Na tujiridhishe kwa pande zote kujitetea .
 
Mkuu that is ma Point......kuwa kwenye Chama ni HIYARI......watu wikikihama chama itakuwaje......? ushawishi wa chama kwenye maamuzi ukoje kama hakuna kujadiliana kutoka ngazi ya chini.........Mnaamua tu huko juu utafikiri chama ni chenu pekeee haya tutaona kinachoendeleaaaaaaaaa......................
 
Historia inaonyesha vyama vingi vikongwe vilitetereka baada ya kupunguza hoja zenye ushawishi. Walizoeana,wakadharauliana,wakafukuzana,ikawa mwisho wao. Mfano ni KANU
 
Ni kweli Mkuu na kingine ni kujiona ya kuwa Chama ni mali yao na wanaweza kuamua chochote bila kupata maoni kutoka kwa wenye Chama ambao ni Wanachama.............Mwisho watu uamua kikihama Chama................Niamini mimi kwenye hili wengi wataondoka na walio madarakani huku ngazi ya chini hawataki tena kugombea Nafazi za uongozi..........Kisa kushurutishwa wakati wapo kwenye chama kwa HIYARI....................!!!
 
Hoja zako nimezipenda!
 
Back
Top Bottom