Ushauri kwa askari wetu wa miamvuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri kwa askari wetu wa miamvuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Inkoskaz, Jun 13, 2012.

 1. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Wakuu
  Nikirejea sticky thread ya marehemu mheshimiwa Regia nadhani pia nivema tukawa na thread yenye kuchangia maoni yetu kwa wizara mbalimbali ili nasi tusio na access na jukwaa la kusemea huenda tukasikika humo na ukizingatia JF ni mkusanyiko wa kada mbalimbali kama wachumi,madaktari,wahandisi,walimu,wanasheria,wafanyabiashara,wanasiasa,wanafunzi,wakulima,wafugaji nk
  hivyo kila wizara haiwezi japo kupata wachangiaji wa kutoa maoni na hata kukosoa inapobidi
  JF ina forums mbalimbali ambazo si rahisi kuzipitia zote hasa kwa mtu mwenye majukumu mengi ya ngazi ya uwaziri hivyo si vibaya waheshimiwa hawa tukiwatumia salamu katika kapu moja na wao wakipitia kila mmoja aokote chake
  Yangu ni machache lakini natumaini yatafungua njia ya wengine wenye mengi kuchangia ili kusaidiana kujenga taifa letu kwa kila mmoja wetu kuwajibika na kusahau ule wimbo maarufu tuliouzoea wa kulaumiana
  Wizara ya Uchukuzi
  Naanzia kwako mh Dr Mwakyembe kwa kuwa naona kuna madudu mengi humu na kama yakifanyiwa kazi tunaweza kujikwamua kwenda mbele
  1.Reli yetu ni mhimili mkubwa wa uchumi,hatuna sababu ya kufikiria kujenga reli mpya wakati hii ya sasa ipo na ni NZIMA ila imeota majani tu,tuiimarishe,izalishe ndipo tutajenga reli nyingine kwa mapato ya hii
  ni kuweka mkazo tu wa kusafirisha mizigo ya Containers na tanks kuwa ni kwa reli pekee kuliko haya malori ambayo kutwa kuchwa yanasababisha ajali(maana mengi ni used na madereva wake hawajapitia mafunzo) na kumaliza maisha ya watz na pia kuharibu barabara zinazotugharimu mabilioni ya shilingi.Nina mfano hai wa barabara ya singida to mwanza maeneo ya sekenke yameshaharibika kutokana na malori haya yanayopitisha mizigo kwenda nchi za wenzetu
  na kutuachia mashimo
  tuache barabara zitumike kwa magari ya abiria na mengine lakini sio mizigo mikubwa
  2.bandari ni eneo ambalo pia linapoteza pesa mingi sana,nchi za wenzetu bandari na reli huwa pamoja ili mzigo ukishuka majini unaingia relini mpaka kwa mteja.lakini hapa ni kinyume bandari wanatoa mzigo wanakata fee zao za vidola tanotano then mzigo unaenda kusafirishwa na watu wanaochaji dola 5000 kwa kontainer! Hizo ni kasoro kwani mapato hayo yasingepotea iwapo reli na bandari zingekuwa pamoja
  Msongamano tulio nao bandarini hasa magari hauna sababu na wala hiyo bandari yenu mpya hatuihitaji,wekeni mfumo mzuri wa kutenganisha huduma.meli za magari zishushe bandari ya Tanga then yaletwe kwa means nyingine,ikiwamo hata reli ya tanga
  Dar port ibaki kwa containers na mafuta na sio kutujazia bandari kavu(ICDs) kila kona,maana naona sasa hadi mjini kati kama pale kamata na veta na serengeti na uda pia,kwa mwendo huu miaka mitano ijayo dar nzima si itakuwa bandari kavu? Tutaishi wapi malori yanalala kila mahali,hebu angalia kurasini,tabata reli na kule TRH sabasaba.hii ni kero sasanchi yetu kupitia wizara hii inapata nini? Tunawafaidisha wageni tu huku sisi tunazidi kudidimia
  3.Ndege
  huku nakuachia naona kuna mipango unafanyafanya japo ina mikingamo lakini ili unreakthrough ni lazima kukanyaga miba tutajitibia mwisho wa safari

  Wizara ya fedha
  Hodi kwako profesa na profesa yule wa Central Bank
  hapa sielewi kwa nini tunakumbatia misamaha ya kodi kwa wawekezaji wanyonyaji wa madini na sekta nyingine.hatuna sababu ya kutoa misamaha hata mmoja kwa hawa looters
  tumeshuhudia ile hotel ya kule Gymkhana ikibadilishwa majina from Sheraton-Royal Palm-MovenPick na sasa Serena kwa kisingizio cha uewkezaji...je hamlioni hilo na kulifanyia kazi??

  Wizara ya Nishati na Madini
  Tumeahidiwa mara kadhaa marekebisho ya mikataba ya migodi,hivi hili ni jambo la siri?mbona hatujifunzi hata kwa jirani zetu botswana? Hata kwa ule mtindo wetu uliozoeleka wa copy and paste bado tungeiga kwao tungenufaika
  Sekta ya umeme ndio haieleweki,inashindikana vipi kuongeza vyanzo vya umeme? Tuna makaa ya mawe,upepo,thermal na gesi lakini hakuna mpango ulio wazi na wenye time frame hata tuwe tukihoji milestone ilipofikia,ni kuahirisha matatizo tu kila siku na sasa umeme ni kama bei ya dhahabu nahivyo kila uzalishaji umepanda ghrama na kuwaomgezea wananchi ugumu wa maisha huku nyinyi taasisi zenu hata bill hazilipi
  Mali asili na utalii
  Hapa kuna meengi sana lakini nawachia wenzangu watakujuza Mh Kagasheki
  Maoni ni mengi sana hasa wizara kama Afya,Elimu,Mambo ya ndani,Kilimo,Uvuvi na ufugaji,ujenzi na wizara ya sheria na katiba bila kusahau TAMISENI Na wizara ya afrika mashariki
  Maoni na kero ni vingi,niishie hapa ila karibuni kwa michango mbalimbali kwa wizara tofauti
  Wasalam
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Wizara ya Afya
  Mfumo wa direct funding from donors haufai,kuna mchwa wanatafuna misaada.mfumo wa kuwaacha wafadhili watekeleze miradi na kuwakabidhi ndio unafaa lakini mkiletewa mafungu hamkamilishi miradi na pia mnadivert funds husika
   
Loading...