Nadhani wanaoendesha hizo e-commerce ama wanakosa ubunifu au sheria na taratibu haziruhusu/hazipo au zina complication sana au changamoto ya kimfumo
Kuna vitu vitatu muhimu ili kukamilisha biashara hii
1. Online platform
2. Malipo
3. Usafiri
Online platform; MayuBey
Malipo; Azam Pesa
Usafiri; Posta/mabasi
Sasa hapa itategemea biashara yako unauza vitu vyako tu au watu mbalimbali watakua wanatumia platform yako kuuza vitu vyao pia
Juma Mtwara akinunua Asali kutoka kwa Lisu Singida kupitia Mayubey atafanya malipo Azam Pesa baada ya kupata reference no kutoka Mayubey
Malipo ataya hold Azam Pesa hadi mzigo umfikie Juma Mtwara ndio Lisu Singida atalipwa
Itategemea usafiri utakua umepangwa vipi
Ama Lisu Singida atalipia na atarudishiwa hela yake ya usafiri atakapolipwa au kutakuwa na mkataba maalum na makampuni, Lisu atapewa ref No atapeleka post na posta watapokea mzigo na kuusafirisha na watalipwa na Mayubey(changamoto ni miundombinu ya namna ya usafiri labda yupo kijijini nk)
Azam Pesa atafanya malipo kwa Lisu Singida baada ya mzigo kufika kwa Juma Mtwara na akaridhika na Mayubey kutoa go ahead alipwe
Then Azam Pesa atakata asilimia yake labda na kodi kisha iliobaki ataingiza Mayubey
Changamoto hapo ni namna ya ku sync kati ya Mayubet app/seller/buyer, Azam Pesa na msafirishaji(hapo vitu vinafanyika online)
Mchakato wote huu anayetakiwa ku initiate ni Mayubey
Halafu sasa baada ya hayo kukamilika inakuja issue ya UAMINIFU
Je Lisu atatuma asali aliyoiyaka Juma?
Je juma atakua mkweli bidhaa aliyopata ipo ok au ataleta usumbufu tu?
Kwa mfano Ebay na Amazon seller wengi huwa hawataki ku ship nchi za dunia ya tatu kama Tz kwasababu ya usumbufu wa buyers wa huku
Mtu hasomi vizuri descriptions za bidhaa anaagiza tu halafu ukifika ana complain
Naamini hawa Jiji wangekuwa serious wakawafuata Azam au mpesa wakayajenga naamini inawezekana kabisa
Kisha wakayajenga na mabasi au posta.... mambo yangekuwa si haba
Aisee umefafanua vizuri kabisaa sasa nikujibu ili uongeze nyama na madini
1.Nia yangu ecommerce hii sio kuuza vitu vyangu kabisaa labda itokee kwa bahati mbaya.Ila nia ni User kupost vitu vyake selller na bayer wakutane
Mpango kazi:
Kutokana na changamoto ya kununua vitu huko IG,whatsapp au kokote kuonekana na wizi mwingi.Ndio sasa linapokuja hili wazo la kuanzisha ecommerce ambapo seller atakutana na Buyer atakua na uwezo wa kuchat nae vizuri kabisa na hata kumpigia.
Changamoto:
Njia ya Malipo ambayo seller atapokea pesa moja kwa moja bila kupitia kwa mtu ILA tu kwenye hayo malipo kuna asilimia kadhaa inakwatwa na kampuni(ecommerce)
Pili,Kutokana na kutoaminiana Naona App hii kuwe na feature ambayo kabla ya seller kupost bidhaa zake.Awe amepitia vetting ikiwemo verification ya kitambulisho cha Nida,TIN n.k hapo ndio mfumo utaapprove kama seller ni genuine au LA.
Tatu,Kutakuwa na feature ya REVIEW kwa seller kama kawaida.seller mwenye review nyingi nzuri atajiweka nafasi nzuri ya kuuza zaidi bidhaa zake.Seller mwenye review ndogo atawekwa kikaangoni.Ikiwemo kumfutia ID(account) yake kwenye database ikibainnika utapeli wa aina yoyote.
Nne,Feature nyingine ni Seller ataweza kulipia Blue tick na kampuni ikiapprove ni genuine itampatia Bluetick na kumuongezea premium features kama vile bidhaa yake kuwa promoted as top ads
Tano:Technology nayopanga kutumia ni Flutter,sqlite,php,js,react,next js n.k ila itakuwa App based tu kwa kuanzia.Halafu badae ndio tutaweka na website.
Mwenye chochote cha kuchangia karibu tukamilishe ndoto hizi wakuu..KARIBUNI