Hujaelewa ila vile umeuliza naomba nikujibu .....
Cm30 ni kina cha shimo kwenda chini sio kina cha kupanda yaani unatifua kusaidia mizizi kupenya kwa urahisi kwenda chini zaidi. Ni sawa na unapopanda zabibu wanachimbo hadi kiunoni wanavyosema wao kisha kuweka mbolea kwa matabaka kama 2-3 lengo ni hilohilo kuifanya mizizi ipate chakula na kupenya kwa urahisi.
Niliwahi kwenda semina moja tukafundishwa nyanya inatakiwa uchimbe kina futi moja na nusu na futi [cm30] iwekewe majani makavu ya nafaka au miti. Kisha weka udongo.
Mdogo sana kisha mbolea ilichanganywa na mchanga kisha panda nyanya yako.
Lengo ni kwamba ndani ya mwezi zile nyasi kule chini zitaoza na kuwa mbolea pia zitakuwa zinahifadhi unyevyu wa kutosha.
Nyanya zilizaa sana mkuu kwenye shina moja nilikuwa nahesabu hadi 211 matunda hayo! Na nililima mashing 517 tu watu walisomba mno.
Hata sasa huaa napanda mashing kama matano5 kaa ajiri ya matumizi ya nyumbani japo huwa sipigi sumu wala mbolea za viwandani lkani huwa nahesabu matunda hayapungui 80!