Ushauri kuhusu KILIMI

ram

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
9,329
8,511
MziziMkavu, barca, Ze marcipolo na madoctor wengine mnahusika hapa

Kilimi(kidaka tonge)changu kimerefuka sana na kina nisababishia kikohozi cha mara kwa mara hasa usiku, nakohoa hadi nakasirika, nimesikia na kuambiwa kuwa dawa ya kilimi kikirefuka ni kukikata, binafsia naogopa mno wala sifikirii kwenda kukikata, nikaambiwa tena kwamba nikiacha hivyo mbali na kikohozi kitakuja kupasuka

Hebu nipeni dawa mbadala ya kilimi instead of kwenda kukikata
 
Ningelikushaui nenda Hospitali kuu ya hapo unapoishi kama upo Dar nenda Nuhimbili ukafanyiwe uchunguzi usiende kwa waganga wa kienyeji tafadhali ram
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: ram
Ni kweli kimeo kama kimeo (Uvula) hakihusiani na kukohoa wala hakihitajiki kukatwa.

Lakini kimeo kiko very vulnerable kwa infection na hivyo hupelekea ku swell, kiki swell sababu ya infection huweza hata kupelekea kufanya usaha (pus) wakati mwengine kina fanya kioteo sababu ya hiyo infection, hicho kioteo ndicho kinacho pelekea kikohozi sababu kina habour virus na bacteria kama vile streptococcus pneumoniae na wengine wanaopelekea kikohozi, hichi kioteo huwa mara nyingi hakipotei kwa treatment za kawaida, hadi kikatwe (uvulectomy)!

Ukataji huo wa kimeo tumezoea kuufanya kienyeji (sishauri iwe inafanyika hivyo, kwa kuzingatia mazingira hatarishi ya HIV, pia uwezekano wa kupelekea magonjwa mengine ya infectio kutokana na mazingira husika), ningeshauri wagonjwa wa vimeo wapelekwe hospital wakapate matibabu katika mazingira mazuri.


Lakini mara nyingi ugonjwa wa kimeo huchanganywa na epiglotittis ambayo nayo pia treatment yake ni sugery na dalili zake ni kama hizo za kimeo, ila hii epiglotittis ni hatari zaidi kwani hu grow hadi kuzuia upumuaji wa kawaida hivyo mgonjwa kukosa hewa na hatimae kufa!




 
  • Thanks
Reactions: ram
Ahsante kwa ushauri mzizimkavu, binafsi sifikiri kukikata, kwani naogopa mno, nitakwenda Bugando hospital kuonana na ENT surgeon, thanks na ubarikiwe sana
 
Kuna mshikaji aliniambia dada yake alikata kienyeji, eti wanaingiza uzi afu wanavuta mpaka kinakatika. Sikushauri ufanye ivo.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Back
Top Bottom