Ushauri kuhusu gari ya kununua

lubamba

JF-Expert Member
Jan 13, 2015
947
614
Wajuzi naomba ushauri baada ya kujichanga na ni mpya ktk kumiliki usafiri. Lipi gari zuri kwa matumizi private, ukizingatia uchumi pande za spare, durability, running expences kati ya prado, harrier na kluger.
 
fafc5fd2cdd9dbbd79605529c91fc572.jpg
Nunua mkwaju uwoo. .......weka mbali na watoto.
 
Unapotaka kununua gari ni vyema kuzingatia yafuatayo;
1: Una nunua gari litumike kwa matumizi gani,labda matumizi ya kifamilia...kibiashara....kioffice..etc
2: Una fedha kiasi gani
3: Unatumia gari hilo katika mazingira yapi
4: Unataka gari lenye sifa zipi;mfano body type Ipi....SUV,hatchback,sedan,saloon,pickup,van na nyinginezo...,Unataka transmission type ipi ; Manual au automatic au semi automatic.,Unataka gari lenye cc ngapi,labda 1290cc,1500cc,2490cc etc...na sifa nyinginezo kulingana na wewe unavyotaka muonekano wa gari lako liwe.
5: Kwa developing countries kama Tanzania wanunuzi wengi hununua used cars kutoka developed countries kama Japan, Uingereza na UK, hivyo inashauriwa unaponunua used car ni vyema sana kununua gari lenye low mileage isiyozidi 75000km....jinsi mileage inavyokuwa ndogo ni kiashiria cha awali cha ubora wa gari lako...

Ni matumaini yangu utakuwa umejifunza kitu..
 
Huu wa kizaman 2008/9 mwambie achukue hii mashine
a5c3a845cc15a8228e0dc786e9b85289.jpg
1a91ee2a183b65ecd6694a6ebcf3caef.jpg
2766fbf783cdd34a48f6be589da78261.jpg


Moja wapo kati ya hizo,,,usiogope kuhusu spare wala ulaj wa mafuta,,ukinunua gar umejiandaaa
Mkuu unafanya inda sasa :D kama nini achukue S class au 7 series 2015
 
Nawashukuru wote mlionipatia ushauri, nilitaja kati ya magari hayo kutokana na mazingira nayoishi.Most of the time ngoma itatumika kwenye rough road ndo maana sikutambulisha saloon cars kwenye uhitaji.Karibuni tena kwa ushauri na matumizi ni private use ikiwa sku nyingine nasafiria kwenda mbali zaidi ya 800 km.
 
Ubaya wa crown ipo chini sana kiasi kwamba kwenye barabara zetu za uswahilini gari unakua unaitesa
 
Mambo yako mazuri unamiliki gari kwa mara ya kwanza unachagua kati ya prado,kluger an harrier?

Hata hivo ili usaidiwe vizuri kuna mambo unatakiwa uweke wazi.

1;Mazingira yako unayoishi na matumizi ya hilo gari kwa maana ya mizunguko yako ya kila siku.
2;Bajeti yako ya kununua gari ni kiasi gani, hapa tutakusaidia ununue gari ya mwaka gani(generation ya gari)
3;Una uwezo wa kuweka mafuta ya kiasi gani kwa siku.

Note; kwa vipaombele ulivoainisha kwenye swali lako mimi naona hayo magari yote yana sifa sawa, ila yanazidiana kidogo
1;harrier
2;kluger
3;prado
lakini kwangu mimi rav4 ndio chaguo langu ukiniuliza m15 hadi 17 unawezamiliki rav4 ya kati mwaka 1998 hadi 2002
 
Back
Top Bottom