Ushauri kuhusu Access bank

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
278
Leo asubuhi nilipokuwa ofisini kwenye Hoteli yangu mara nikagongewa na mfanyakazi wa Hoteli na kunijulisha kuwa kuna mgeni anaomba kuonana nami. Bila kusita nikamkaribisha. Alipongia akajitambulisha kuwa anatoka Accessbank na ni Afisa Masoko.

Akanieleza faida ya kuwekeza fedha katika Benki hiyo kwa nyakati mbali mbali.Mfano ukiwekeza Tshs. 100,000,000 kwa siku 30 unapewa faida ya 16.0%, miezi miwili faida ya 16.3%, miezi mitatu faida ya 16.6%, Miezi sita faida ya 16.9%, miezi tisa faida 17.2%, na mwaka faida ni 17.5%. Lakini nilipoulizia NMB wenyewe wanaweza kutoa faida kati ya 7.5 mpaka 10%. Huyu Afisa Masoko akanieleza kama leo hii nikiweka hizo hela wataniongezea 1% kwa kila muda nitakaoweka fedha hizo. Mfano kama faida kwa mwaka moja ni 17.5% wenyewe wataniongezea iwe 18.5%.

Naomba kuwauliza je Benki hii ni mahala salama nikiwekeza fedha zangu kama Tshs.200,000,000?. Je credibility ya Benki hii ikoje?. Kama watu wanaowekeza fedha zao na kupata faida kama hiyo, Je watu watakaokopa kutoka kwenye Benki hiyo watalipa riba ya kiasi gani?. Huoni kama wananchi wa kawaida ndiyo wataumia kutoka kwa wale waliokopa kwa riba kubwa na baadaye kupandisha bei ya bidhaa zao?.

Naomba ushauri wenu,Je Benki hii ni mahali salama pa kuwekeza?. Isije ikawa kama DECI.
 
Leo asubuhi nilipokuwa ofisini kwenye Hoteli yangu mara nikagongewa na mfanyakazi wa Hoteli na kunijulisha kuwa kuna mgeni anaomba kuonana nami. Bila kusita nikamkaribisha. Alipongia akajitambulisha kuwa anatoka Accessbank na ni Afisa Masoko. Akanieleza faida ya kuwekeza fedha katika Benki hiyo kwa nyakati mbali mbali.Mfano ukiwekeza Tshs. 100,000,000 kwa siku 30 unapewa faida ya 16.0%, miezi miwili faida ya 16.3%, miezi mitatu faida ya 16.6%, Miezi sita faida ya 16.9%, miezi tisa faida 17.2%, na mwaka faida ni 17.5%. Lakini nilipoulizia NMB wenyewe wanaweza kutoa faida kati ya 7.5 mpaka 10%. Huyu Afisa Masoko akanieleza kama leo hii nikiweka hizo hela wataniongezea 1% kwa kila muda nitakaoweka fedha hizo. Mfano kama faida kwa mwaka moja ni 17.5% wenyewe wataniongezea iwe 18.5%.
Naomba kuwauliza je Benki hii ni mahala salama nikiwekeza fedha zangu kama Tshs.200,000,000?. Je credibility ya Benki hii ikoje?. Kama watu wanaowekeza fedha zao na kupata faida kama hiyo, Je watu watakaokopa kutoka kwenye Benki hiyo watalipa riba ya kiasi gani?. Huoni kama wananchi wa kawaida ndiyo wataumia kutoka kwa wale waliokopa kwa riba kubwa na baadaye kupandisha bei ya bidhaa zao?. Naomba ushauri wenu,Je Benki hii ni mahali salama pa kuwekeza?. Isije ikawa kama DECI.
ACCESSBANK NI SALAMA KUHIFADHI HELA ZAKO NA WAKO TRANSPARENT KULIKO BANK NYINGI, WANA KPMG AWARD YA CSR
 
umejuaje/umeaminije huyo aliyekutembelea anatoka access bank? una mil 200 uje kutafuta ushauri JF? acha mzaha. na ippmedia ulishaacha kazi lini hadi ukamiliki hotel ya kukuingizia mil 200?
 
Back
Top Bottom