Ushauri: Kesho CHADEMA wabebe bendera za taifa

Ushauri: Kesho CHADEMA wabebe bendera za taifa

Tangopori

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2012
Posts
1,628
Reaction score
1,289
Wanabodi,
kwa upande wangu ningeshauri kesho kwenye hayo maandamano yanayosemekana kuwa ya wapinzani wote waliokubali mwaliko kutoka chadema basi ningeshauri zibebwe bendera za taifa lakini nguo za vyama zibaki zilezile za kawaida kama magwanda na scarf.
Huo ndo ushauri wangu!
 
Ni jambo la msingi sana..nashauri viongozi walifanyie kazi
 
Nafurahi umechukua mchango wangu na kuanzisha thread, nnakuunga mkono,
Nashauri kwa WAJASIRILIAMALI kutumia hayo mapokezi ya MAJEMBE yetu kama opportunity kwa kuleta bendela za taifa na kuziuza, binafsi ninayo ya kwangu, kuna jamaa zangu wametafuta leo ila wamekosa kwa wanaoweza kupata na kuja kuziuza zitauzika kwa wingi saana, kwa waelewa wameelewa ni nini nnamaanisha

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?p=5650482
 
Tatizo hizo bendera za Taifa tutazipata wapi kwa masaa machache haya yaliyobaki, istoshe serikali yetu haina utamaduni wa kuruhusu wananchi wake kuwa na bendera ya taifa labda iwe ktk ofisi au shule za serikali au gari la kiongozi wa serikali.

Ndio maana unaweza kukuta nyumbani kwa mtu kuna pazia ambalo ni bendera ya marekani au Uingereza na si bendera ya tanzania.

Tunaishi tukitukuza nchi za watu kuliko ya kwetu.
 
Wazo bovu kabisa. Yaani bendera ya taifa ni ya kuidhalilisha hivyo?
 
Wazo bovu kabisa. Yaani bendera ya taifa ni ya kuidhalilisha hivyo?

Mkuu, bendera ya Taifa ni nini?...ni wapi au kwa matumizi gani utaidhalilisha?

Ni ukweli hatuna utamaduni huo, lakini hatuna utamaduni huo kwa sababu ya kuendekeza vyama mbele na utaifa nyuma(baadae).

Sasa, hebu fafanua pale mikutano ya kisiasa yenye nia njema kwa wafuasi/mashabiki kutumia bendera ya taifa(kama raia wa nchi hii) UDHALILISHAJI uko wapi?

Ni kwa mifano ipi(ya Nchi Afrika na Nje ya bara hili) Utumiaji wa bendera ya Taifa(ya nchi husika) katika mikutano halali ya kisiasa, na kwa watu wenye nia njema ilihesabika/kuchukuliwa kuwa ni UDHALILISHAJI?
 
polic mkoa wa tmk wamepiga marufuku hayo maandamano. source.radio times.
 
Wazo bovu kabisa. Yaani bendera ya taifa ni ya kuidhalilisha hivyo?
Muulize Mwigulu anaeiba wake za watu na bendera yaTaifa shingoni....!acha Chadema waonyeshe uzalendo wao kwa taifa. naunga mkono wazo.!
 
Tatizo hizo bendera za Taifa tutazipata wapi kwa masaa machache haya yaliyobaki, istoshe serikali yetu haina utamaduni wa kuruhusu wananchi wake kuwa na bendera ya taifa labda iwe ktk ofisi au shule za serikali au gari la kiongozi wa serikali.

Ndio maana unaweza kukuta nyumbani kwa mtu kuna pazia ambalo ni bendera ya marekani au Uingereza na si bendera ya tanzania.

Tunaishi tukitukuza nchi za watu kuliko ya kwetu.

mkuu kama sikosei kuna zile ambazo zimetengenezwa kama vitambaa, zinauzwa na wamachinga kariakoo
 
Back
Top Bottom