Ushauri jamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri jamani

Discussion in 'JF Doctor' started by R CHUGGA, Feb 24, 2012.

 1. R CHUGGA

  R CHUGGA Senior Member

  #1
  Feb 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naomba ushauri wenu katika hili!
  Ngozi ya korodani inapokuwa inatoa kitu kama fungus-yani ngozi inakuwa kama ina magamba halafu ni upande mmoja tu,katika korodani la kulia.
  nimetumia sabuni nyingi za ngozi lakini bado inaendelea.
  Hivi hii inasababishwa na nn hasa na nini tiba yake?
  Nahitaji ushauri na sio masihara.
   
 2. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Hizo zitakuwa ni fungus tiba chakwanza nunua dawa inayoitwa Quadriderm cream 15 g yenye composition batemethasone (as 17-valerate) 0.5 mg,gentamycin (as sulphate) 1mg ,iodochlorhydroxyquin 10mg na tolnaftate 10mg hakikisha unatumia mara mbili kwa siku within 2wk .cha pili nunua Deltol fua nguo zako zandani kwa deltol hakikisha unakuwa msafi
   
 3. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 706
  Trophy Points: 280
  tatizo hilo lipo kwa watu wengi na huwa hasa ni fungus hivyo kule hospitalini huwa tuna vipimo ambavyo tunaweza kujua nini tatizo lako na pia tatizo lako huwa linasabishwa na aina nyingi za fungus hivyo matumizi ya sabuni kamwe hayawezi kukupatia matibabu sahihi hivyo fika kituo cha afya cha uhakika kama[selian kama upo r chuga] ili kupata ufumbuzi zaidi kwani korodani jombaa ndo bunge la tz
   
 4. G

  Goodnes Member

  #4
  Feb 27, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 91
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  pole kaka! Huenda ikawa ni fungus,cha kufanya nenda hospital or phamarcy yenye wataalam watakupati cream ya fungus utapaka, pia kuna vidonge inategemea ukubwa wa tatizo.
  ILA ukiwa unatumia hiyo dawa zingatia usafi wa nguo zako za ndani kama ifuatavyo, ziloweke kwenye maji ya mto sana na uzifue zote hata kama ni safi,ukishindwa zifue na uzianike kwenye jua kali kwa muda mrefu,auzifue zikikauka zipige pasi kwa moto mkali,hii itaua wadudu wote walioko kwenye nguo zako,
  cHA pili, badilisha chupi kila unapooga kisha ifeu na kuiinyoosha..
  cHA tatu usirudie chupi na hakikisha mara nyingi unakuwa mkavu. Pia epuka maambukizi mapya ya fungus mfano kutoka kwa ulienaye au mashuka baadhi ya gest house wasizozingatia usafi,
  Kwa kufanya hivyo kila siku, fungus hizo utazisikia kwa jirani maana zipo watu wengi zinawasumbua si wanawake wala wanaume.
  GET WELL SOON!

  Note; niliposema mashuka ya gest house simaanishi lazima wewe unakwenda huko huo nimetoa ushauri wa general.(wa pamoja) kwa kila atakae soma na kuona ushauri huu unamfaa.
  Asante
   
 5. n

  ngilenengo1 JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 933
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Ushauri mzuri kwetu wote, tuuzingatie
   
Loading...